Jesli la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu sita ambao wanajihusisha na vitendo vya kishirikina kwa kujifanya wanaagua na kufichua watu wachawi katika vijiji mbalimbali. Wanaenda mbali zaidi na kudai wanafichua watu wachawi wanaozuia mvua isinyeshe katika maeneo mbalimbali hapa Dodoma. Watuhumiwa hao hujulikana hapa Dodoma kwa jina maarufu LAMBALAMBA. Watuhumiwa walikamatwa tarehe katika kijiji cha MBALAWALA.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akielezea ukamatwaji huo na kuonesha tunguli walizokuwa wanatumia




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Utamaduni wetu huo sio ushirikina

    ReplyDelete
  2. Bongo bwana, bado inaaminika kwamba binaadamu anaweza kuzuia mvua isinyeshe, au kutengeneza radi, kufa na kufufuka kisha kurudi nyumbani.
    Inatia huzuni kweli masikini.

    ReplyDelete
  3. Hizo ni evidence za ushirikina?

    ReplyDelete
  4. Swali je Serikali inaamini uchawi?? Mimi binafsi naona Kamanda wa Polisi Dodoma hana kazi ya kufanya na anatafuta umaarufu hapa kwenye globu letu la kimataifa badala akamate majambazi na kuzuia uharifu yeye anaenda kukamata waganga feki!! Au na yeye mchawi na ana amini uchawi/ushirikina!! Hacha kuuza sura mkuu ili mradi tu wazee makao makuu wakuone!!

    ReplyDelete
  5. Alichofanya Kamanda ni sahihi, naomba nikujuze Anonymous Sat Apr 20 10:50:00am 2013. Nikufahamishe tu kwamba huko Dodoma kuna waganga wanajiita LAMBALAMBA wanashika watu kwa uchawi na mbaya zaidi wanafanya watu wauwane sababu alimroga mwenzake KWA MAANA HIYO Police wameingilia kati kuwakamata hao LAMBALAMBA ili kurudisha Amani kwa watu na kuzuia mauwaji ambayo yanasababishwa na hao waganga. Kwa upande wangu naona walilolifanya ni jambo la busara kuzuia kufunjisha Amani.

    ReplyDelete
  6. ukiamini Mungu yupo amini na uchawi upo!!!

    ReplyDelete
  7. Ni wazi kuwa Sayansi hii mara zote inashindwa kutoa Matokeo kuafaka.

    Manaona sasa, jamaa wameendesha weee Operesheni yao wakifikiri uwezo wao ni mkubwa na sasa wapo chini ya Mkono wa Dola, huku walijaribu kumrusha Bundi wakashindwa na sasa wanaona Bundi akiwa amewafia mikononi!

    Je uwezo kweli wanao?

    ReplyDelete
  8. Cha muhimu ni kufanya kazi ya kuijenga nchi sio kuhangika na mambo yasiokuwa na uzito

    ReplyDelete
  9. Kumbuka kuwa hawa ndo wanasababisha pia ma Albino wauwawe na kukatwa mikono. Serikali lazima iingilie mambo kama haya ya upuuzi wa kwenda sijui bagamoyo kulogana na kutafuta kinga...!!

    ReplyDelete
  10. Mimi huwa sielewi huu ni utalaam wetu tungetafuta namna ya kufaidika nao.nadhani wanamambo mazuri y akujifunza toka kwao kwanini tusifanye tafiti nao kujaua uwezo wao na tukautumiasiku moja? nashauri vilevile tuanzishe blog wa wachawi maana tutapata micahngo mingi ya mawazo mimi napaenda kutafiti eneo hili nadhani lina maana katika maendeleo ya karne ijayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...