Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge Corporation MCC Bwana Daniel Yohannes ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Balozi wa Marekani Alfonso Lenhardt.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akioongea na makundi mbalimbali pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama vilivyoshiriki katika zoezi la uokozi wakati wa ajali ambapo jengo la ghorofa liliporomoka , kuuwa na kujeruhi watu kadhaa katikati ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibun.Hafla hiyo fupi ilifanyika katika ukumbi wa Sabasaba katik viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova kwa uendeshaji wa Zoezi la uokoaji katika ajali ya Jengo lililoporomoka jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kijana mlemavu Shabani Selemani Mohamed katika ukumbi Sabasaba katuka viwanja vya maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa ,wakati wa hafla fupi ya kupongeza makundi mbalimbali yaliyoshiri katika kazi ya kuokoa watu na kuopoa miili wakati wa ajali ya kuanguka kwa ghorofa katikati ya Jiji la Dar e Salaam hivi karibuni.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ walishiriki katika kazi ya kuokoa watu wakati wa ajali ya kupomoka kwa jengo katikati ya jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo...kazi hata za polisi ni pamoja uokoaji wa mali na maisha ya raia, halafu wanazawadiwa. Wa kuwazawadia wangekuwa ni watu ambao ni wa kawaida, si wa vikosi vya ulinzi na usalama au red cross. Labda mpita njia aliyeamua kuja kusaidia

    ReplyDelete
  2. Kulikua kuna kijana mmoja habari zake ziliandikwa sana ktk gazeti la mwananchi jinsi alivyojitolea ktk zoezi zima la uokoaji na inasemekana maiti zote ni yeye ndie aliyekua akionesha sehemu zilipo kabla ya kufuriwa, hapa simuoni ktk zoezi hili la kupeana zawadi walau haya picha yake haipo sijui imekuaje??????

    ReplyDelete
  3. Ndugu zangu Watanzania,

    Tuache wivu usio na maana. Kuzawadiwa kwa kufanya kazi vizuri kuna maana kubwa, zaidi ya chakula/kinywaji au pesa anayopatiwa mtu. Watu sio mashine, bosi wangu anaponiambia "asante, kazi nzuri" huwa nafurahi kweli na huwa ananifanya siku nyengine nichape kazi kwa morali. Laiti huyu bosi wangu angelikuwa kila siku hana jema na mimi, kila siku unafanya kazi hakuna asante, ningalivunjika moyo sana.

    Tujifunze kushukuru. Hicho chakula walichopewa jamaa bila ya shaka ilipofika jioni walikuwa na njaa tena. Lakini kupeana mkono na president itabakia katika kumbukumbu.

    ReplyDelete
  4. watu kama dula said ndio mnaoharibu nchi na kuwavunja moyo watendaji, hivi mwanao afanya vizuri katika mitihani yake ukamwambia asante umefanya vizuri endelea ktk mstari huo kuna ubaya gani pamoja kwamba ulikuwa ni wajibu wake kusoma kwa bidii na kufaulu? anachofanya Mheshimiwa Rais ni kuwapa morali wa kufanya majukumu yao vizuri zaidi. kama hatuna

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...