Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akimuongoza kuelekea kwenye chakula cha mchana Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto na mkewe Rachel Chebet katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akipozi na familia ya Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka. PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

Akiongea na mgeni huyo katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara, Rais Kikwete amempongeza Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya.

Mhe Rais pia alimueleza Mhe Rutto furaha yake pamoja na kuridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.

Alielelezea matumaini yake ya kuwa urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya utadumishwa pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe Rutto, ambaye aliwasili mkoani Mara wiki iliyopita akiwa na mke wake na watoto, ameondoka leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mambo poa mkuu kikwete biashara poa kenya lazima ucheke

    ReplyDelete
  2. hivi ni naibu rais au makamu wa rais ...au copy paste...anyway sio issue...hapa watu wa utalii wachangamke kutumia hii visit kama sehemu ya kutangaza utalii wa hapa ndani...

    ReplyDelete
  3. Picha ya 3 juu Mhe. Raisi JK akiongea na Mhe.Ruto Makamu wa Raisi Mteule wa Kenya, inaonekana kama vile JK anamuuliza ulionaje kuhusu habari ya joto la mshike mshike wa Uchaguzi wenu?

    Mhe. Ruto anabaki akiangua kicheko, hahahahaha na kusema ndugu yangu JK we acha tu, si mchezo hivi unavyoniona ni jana tu (Jumamosi) tumemalizia Mahakama Kuu!

    ReplyDelete
  4. Mhe. Ruto, je ktk hao Mabinti zako pana kasichana ka kuoa hapo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...