Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bw John haule  kwa Balozi wa Bangladesh nchini Mhe Wahidur Rahman baada ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa  kwa Balozi wa Kuwait  nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad na Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage  kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  Balozi wa Kuwait  nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam. Kushoto ni Bw Abdul Rahman Al-Hashim, Meneja wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait aliyeongozana na balozi huyo.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho toka kwa balozi wa Slovak Mhe Michal Mlynar   leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Balozi wa Ugiriki nchini Mhe Elefthereios Kouvaritakis baada ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam
PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...