Home
Unlabelled
RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALI HASSAN MWINYI AFAFANUA KAULI YAKE KUHUSU KUCHINJA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Namshukuru mheshimiwa Mwinyi kwa nasaha zake nzuri kuhusu jambo hili. Ninaomba kuonyesha kuwa hata biblia inaongelea kuto kula nyama iliyonyongwa. Matendo 14:20 inasema wazi.
ReplyDeleteAhsante
Mzee Ruksa tunashukuru sana kwa busara zako,lakini naona kama hukumalizia. Umesema dharura ya ndugu zetu waislamu ni kwamba nyama lazima ichinjwe kwa mujibu wa Kurhani, je nani kasema kwamba wakristu hawachinji? Nadhani ningekuelewa kama ungesema Kurhani inakataza nyama ambayo haijachinjwa na muislamu. Hii ingesaidia zaidi.
ReplyDeletePili, nakubaliana na wewe kabisaa, kama miaka yote tumekula nyama iliyochinjwa na muislaamu na hatujagombana, leo nini kimetokea? Mh Mwinyi,ningependa umalizie kusema kuwa, Kurhani inakataza nyama ambayo haijachinjwa na mtu ambaye si muislamu, unless kama hamna hicho kipengele, basi useme hata akichinja mkristo basi ruksa, as long as imechinjwa. Please rekebisha hapa ili kuondoa utata. Pia ungekomelea kabisa kwa kusema, Ruksa kwa watu wote kula nyama iliyochinjwa na muhislam kama ambavyo imekuwa siku zote. Mimi ninayeandika hapa ni mkristu safi, na sipendi hili jambo kabisa. nani katuletea balaa hii. Nianze kuua dada na kaka zangu wa damu, maana familia yangu ni mchanganyiko. Ujinga huu. Asanteni
Mdau hapo juu wewe ni Muislamu jinsi tu ulivyoandika usisingizie Uislamu to support your argument. Mie nadhani watu wana uhuru wao wa kuchinja na kula nyama, sio mantiki yeyote eti Muislamu ndio achinje...nani kasema Mkristu ni kafiri? Wakati bado naishi bongo wazazi wangu walikuwa wanapeleka kuchinja kuku kwa jirani ambaye ni muislamu alikuwa tumezoea kumwita mzee Salum, nakumbuka kaka yangu alikuwa anaishi hapa marekani muda hule, alipokuwa nyumbani likizo aliona house girl wetu anapeleka kuku kuchinjwa nyumba jirani, nakumbuka vizuri kaka yangu alimwambia mama, NO, mlete hapa nichinje tangu siku hiyo baba yangu alikuwa anachinjia. Argument ya kaka yangu ilikuwa kwani Muislamu ni nani? Mie nadhani huu mjadala ni wa kitoto sana na kuwa na mawazo madogo. Mambo ya imani ni ya mtu binafsi. Mbona Korani inawakataza kunywa pombe lakini wengine mnakunywa...acheni wakristu wawe huru kwenye nchi yao wenyewe, Tanzania kama nchi haina dini yeyote.
ReplyDeleteWanaoendeleza jambo hili hawana hoja ya msingi. Miaka yote tumezoea kula nyama inayochinjwa na waislam. tena hata kwetu imekuwa ni mazoea ukijua una shughuli inayohusisha watu wote, unatafuta muislam achinje. tumeishi ivi tukiheshimiana miaka yote. Hoja hii ya wakristu kutaka kuchinja imetokea wapi? Hawa watu wanaoeneza mambo haya wanatafuta nini? Jamani, Tanzania iliyo moja ni kipaumbele zaidi hata ya dini zetu. Tukipoteza umoja hata hizo dini zenu mtakosa mahali pa kuabudia. Propaganda za kidini hazina mashiko katika dunia ya leo. Kila siku duniani kote watu wanazungumza kuungana, kuwa kitu kimoja, sisi tunaendekeza kuongelea kutengana. Ujinga mtupu...! Kamwe tusikubali jambo hili kuingia katika akili zetu. Tuwaambie wanaoeneza jambo hili hatutaki. Tunataka kuendeleza nchi yetu na familia zetu kiuchumi. Tuondokane na umasikini. Hiyo ndio vita yetu. Nna mashaka kuna watu wanataka kutuondoa katika ajenda zetu za kitaifa. Tusielewane ili wao waendeleze wanachokitaka. Tuwe makini ndugu zangu.
ReplyDeleteProsper Magali
Aksante mzee wetu kwa busara zako za kufafanua suala hili, kumbe la msingi ni kwamba ili nyama iwe Halal ni lazima ichinjwe na isiwe kibudu. Sasa tunagombana nini wakati jambo la msingi si mwenye dini gani achinje bali ni nyama ichinjwe ili isiliwe kibudu.
ReplyDeletemjadala mdogo tu, bucha ziwepo za dini mbali mbali na mwenye kupenda anunue nyama popote atakako, ukienda kwenye mikutano ya kimataifa hata buffet utakuta zipo mbili hallal food na ya kawaida tuache kulazimishana , watanzania ni zaidi ya waislam na wakristo wapo WAPAGANI pia.
ReplyDeleteViongozi wa nchi ambao ni waislamu wanapofanya ziara za ulaya, Asia, America, an Australia na kuhudhuria dhifa za kimataifa huwa wanafuatana na wachinjaji wao? Kama sivyo, nyama wanazokula huwa zimechinjwa na nani/nini?
ReplyDeleteMdau wa tatu mwenye kaka na inaelekea nawe pia unaishi ughaibuni.
ReplyDeleteNaona umekurupuka. Mzee ruksa amesema wazi na nadhani ilikuwa inaleweka toka enzi za zamani kua Mkristo anaweza kuchinja ili mradi ni kwa matumizi yake binafsi na familia yake au na marafiki zake. Kinachosemwa hapa ni kuwa na mabucha ambayo Mkristo amechinja.
Jamani tulikuwa tunaishi kwa amani bila tatizo lolote kati ya Wakristo na Waislam. Tunajumuika kwenye kila aina ya shughuli, toka maharusi hadi kuzikana. Lakini kwa kuheshimiana na kustahi imani za waIslam inapofanywa karamu au mlo. Hata kutembeleana majumbani kwa kualikana, Muislam anakuwa hana hofu yoyote ile kuwa atalishwa nyama ambayo haikuchinjwa kwa itikadi za Kiislam. Kwa kweli tunataka tuvuruge yote haya kwa ajili ya ujinga wa watu wachache tu?
Wanaoshikilia hili wanataka kuua uhusiano na uwiiano wote kati ya Waislam na Wakristo??
Ukiishi ughaibuni, ni tofauti na kabisa na Tanzania. Jamii huwa ndio mhimili wa maisha kwa ujirani na urafiki bila kujali udini. Jamani tusipande mbegu ambazo mavuno yake tutayajutia. Kama alivyosema mzee Mwinyi.... Tukianza na hili, halitaishia hapo.
Mungu tubariki Watanzania. Wakristo, Waislam na waumini wote wengine.
Wadau, alichokizungumza baba Mwinyi kipo sahihi ki-mazoa. Lakini ki-sheria siyo sahihi hata kidogo. Na siku zote mazoea si sharia. Ki-sharia, serikali isiyokuwa na dini, vitabu vitakatifu havina nafasi kuamua nani achinje na nani asichinje mnyama kwaajili ya biashara. Hayo yanaruhusiwa katika serikali za kidini na zile za kiimla. Kama wakristu wapo tayari kuchinja kwaajili ya biashara zao sharia ya nchi inawaruhusu na hakuna sheria inayowalazimisha waislamu kununua nyama hiyo. Na kama waislamu wameamua kuchinja kwaajili ya biashara, wanaruhusiwa na wakrustu hawalazimishwi kununua nyama hiyo. Sina tatizo na waislamu kuchinja wanyama kwaajili ya biashara nchi nzima, lakini naomba ieleweke kuwa hakuna sharia yeyote ya nchi inayozuia wakrustu kufanya hivyo pia.
ReplyDeleteSurat maidah 5: 5 This day [all] good foods have been made lawful, and the food of those who were given the Scripture ( Jews and Christians ) is lawful for you and your food is lawful for them.
ReplyDeleteAccording to Ibn Abbas, the food of the People of the Book (jews and christians) mentioned in Surat maidah 5:5 refers to the meat slaughtered by them.
ReplyDeleteBased on this, the majority of scholars belonging to the four schools of thought consider it permissible for Muslims to eat animals slaughtered by the Christians and Jews so long as these animals are considered lawful for us to eat.
If you fall in this category of those who live among the People of the Book ( Jews and Christians ), then you may eat their meat especially if you cannot find meat slaughtered by Muslims.
Nyinyi watu mna matatizo na yanapokuja maswala yasiokuwa na msingi kama haya hakuna wataalam kama watanzania. Nchi iko miaka 200 nyuma kimaendeleona sababu zake nyingi ziko wazi miaka nenda rudi tunasumbuliwa na swala la incompetence na kukosekana uwajibikaji na wahusika wakuu wanajulikana baada ya kukubali makosa na kujadili mbinu za kuondokana na hayo yanaliyoisimisha nchi kwa miaka 50 iliyopita mnakaa na kuzungumzia na kutaka kuuana kuhusu kuchinja halafu kuna wengine wanakuja na kusema mimi niko marekani! sasa..peleka ujinga wako wa kitanzania huko marekani uone watakufanya nini. Nchi nyingine kuna mabucha ya halal na mengineo tatizo ni Tanzania hakutokuwa na nidhamu ya mabucha kuwa sehemu kadhaa kwani wengine wataanza na kusema kwa nini tumewekwa ubungo na segerea na mabucha ya halal yako kariakoo, magomeni na kinondoni hili ndio tatizo moja kubwa mno Tanzania na serikali inatia pamba masikioni na kuziba macho na kusema hakuna tatizo wakati Waziri mkuu anaweza kuja kusema leo kuwa hapa nyama itakayouzwa itachinjwa na waislam naukitaka kuchinja yako kwa matumizi binafsi hiyo juu yako, poa..lakini hatofanya hivyo na baadae hali itakapokuwa mbaya zaidi watakuja in favor ya kundi la wanaojiona wabora hili ni lile kundi linaloamini kuwa lina haki kuliko wengine kumbe ni wabinafsi tu na wakosefu wa ustaarabu kwani kufikisha neno lako sio lazima upige kelele au ugombane. Baada ya miaka 51 ya uhuru kweli leo tunakaa kuzungumzia nani achinje nyama badala ya kwa nini kuna ajali nyingi za barabarani na kwa nini hatuna umeme na pia kwa nini uhalifu nchini haupungui.....
ReplyDelete