Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) aliowaita leo nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam,wakati alipozungumzia swala uhalali wa kuchinja ambalo limekuwa ni gumzo sana hapa nchini kwa kipindi cha hivi karibuni.Mzee Mwinyi ametoa rai kuwa Swala hilo ambalo limekuwa na utata mkubwa na kupelekea kuzua vurugu kwa baadhi ya maeneo hapa nchini,kuwa liachiwe watu wenye dharula kama linavyoelekeza kwenye Moja ya Vitabu vya dini.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wamsikiliza kwa Makini Rais Mstaafu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
 Rais Mstaafu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya waandishi wa Habari waliofika nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo.

TAARIFA KAMILI ITAWAJIA BAADAE KIDOGO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Mimi sioni tatizo liko wapi. Suluhisho ni rahisi kama lilivyo kwenye nchi nyingi duniani. Maduka yanayouza nyama iliyochinjwa kiislamu hubandika neno "Halal meat" na wanaouza isiyochinjwa kiisalmu hawabandiki kitu. Matokeo yake mnunuzi ana hiari kununua duka lolote atakalo akijua ni aina gani ya uchinja umefanyika katika nyama anunuayo. Sasa hapo pana shida gani hasa?

    Mimi binafsi naona issue sio uchinjaji bali ni issue ni uchochezi wa hali ya usalama nchini kwa kutumia dini, Watanzania tujihadhari na haya.

    ReplyDelete
  2. Nadhani suala hili la Uchinjaji linahitaji busara zaidi.

    Je miaka yooote huko nyuma tulikuwa kizani?

    Hivi miaka yote mbona hatukuwa na malumbano kama haya kuhusu Uchinjaji iwe leo?

    ReplyDelete
  3. Hapa wenye jukumu la mwisho kuamua jambo hili ni viongozi wa dini husika, kwa kuelewa kwamba Mkristo halazimiki kula nyama iliyochinjwa na mwislamu na halazimiki kumuita mwislamu amchinjie kitoweo chake na vile vile anaweza kula kilichochinjwa na mtu mwingine.

    Wakati huo huo mwislamu ni lazime ale alichochinja mwislamu mwenzake.

    Sasa kwa kutambua waislamu na wakristo tunaishi kama ndugu, basi ni vyema waislamu wakawaomba wakristo wawaachie wao kuchinja ili wasije wakala kitoweo kisichochinjwa na waislamu na zaidi kuruhusu mchanganganyiko usiokwepeka kama vile mashuleni, misibani, harusini, jeshini, nk.

    Wakristo ni waelewa, haitakuwa tatizo kwani tumeishi hivyo kwa miaka mingi.

    Tatizo litakuwa kubwa endapo

    1. Waislamu watatumia ubabe kwamba ni lazima wao wachinje bila kupata muafaka na wakristo.

    2. Serikali itajaribu kulazimisha Waislamu wachinje

    3. Wakristo waaminishwe kwamba desturi ni sheria wakati utaratibu huu uko kwa nchi kama uingereza

    4. Watatokea wachochezi kama mzee wa Upako kuwaita Maaskofu waliosoma theology kwamba ni wapumbavu wanapogombania kuchinja

    ReplyDelete
  4. Ktk suala la Uchinjaji mzizi wa fitina ni uchu tu!

    Ilikuwa ni mazoea unapomwita Mchinjaji kukuchinjia vitu kama

    1.Shingo,
    2.Vipapatio (kama ni kuku)
    3.Miguu (kama ni kuku)
    4.Makongoro (kama ni ng'ombe au mbuzi)
    5.Mzigo wenyewe yaani....(Mapu,,,w,,,bu) kama mnyama ni dume.

    Bidhaa hizo 5 hapo juu bila maswali wala nini ilikuwa ni mali ya mchinjaji !

    Kulingana na kasi ya maisha kwenda juu sasa Wanao chinjiwa wanamaindi ndio yanatokea haya sasa!

    ReplyDelete
  5. Suala la kuchinja kwa nyama ya UMMA tumelirithi tangu zamani. Wakoloni kama Wajerumani, Waingereza walilikuta na waliliendeleza. Na tulipopata uhuru tukaliendeleza. Tuliendelea kuishi kwa amani kiasi kwamba watu wa itikadi tofauti tulikuwa tukikaribishana kwenye chakula bila kigugumizi. Hii iliendeleza upendo na mshikamano. Tuendelee kulitelekeza kwa faida ya umma.

    ReplyDelete
  6. Zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa nawasikia ndugu zetu Wakristo wakisema kwamba ukiona mkristo anachinja mnyama au ndege basi ujue hataki waislam wale chakula chake kwa hiyo walikuwa wanawaomba waislam wawachinjie ili hata kama akitoa mwaliko kwa ndugu zake Waislam basi nao wajumuike pamoja,lakini sasa imekuwa ni kinyume,tujiulize nini matokeo ya mvutano huu?Je sio mwanzo wa kutengana na hata kususiana shughuli?

    ReplyDelete
  7. Watanzania tunajirudisha nyuma sana..Uchinjaji upo toka karne nyingi zilizopita..na miaka yote hii imekuwa ni waislamu ndio wanaochinja sasa leo hii wanaotaka kubadili hali hii wakati hata ulaya wanatumia Uislamu katika kuchinja..Mi naona hawa wachochezi hawana nia njema katika nchi yetu..hawa wanaotaka kuchinja kikristo wakati imeshazoeleka katika nchi kwamba nyama imechinjwa kiislamu. hayo mambo ya kuandika hii ni halali au si hali naona ni kujitia katika matatizo wakati jawabu tunalo toka karne. Naogopa kuwa watanzania tunaanza kupotoka wakati tulishakuwa waongofu.

    ReplyDelete
  8. huo mjadala naona hauna maana nani aruhusiwe kuchinjwa au nani asiruhusiwe.uku Ughaibuni sidhani kama ata wanachinja na badala yake wanyama wanapitishwa kwenye SHOTI YA UMEME AU WANAULIWA KWA GESI YA CO2,JE MBONA WAISLAMU NA WAKRISTO BADO WANAKULA NYAMA,waishiyo Ughaibuni.kama ndio ivyo basi na sisi uku ughaibuni tungeshaandama kwa vile nyama ilivyopitishwa kwenye shoti ya umeme bila kuchinjwa nayo ni haramu.
    Inabidi tubadilike na kuacha kushabikia vitu ambavyo mwisho wa siku havitupi manufaa
    Mdau.
    PhD student-TOKYO JAPAN

    ReplyDelete
  9. ndugu zangu uelewa ni kitu kidogo sana lakini mtu akishaelewa hapana shida hebu paangalie hapa tanzania inasifika kwa amani lakini haina amani bali ina utulivu tu,kwanini ninani kati ya mwiislamu na mkristo aliye halali na haramu wote sawa katika biblia na quran ni mtu mmoja tu aliyeambiwa na mnyezi MUNGU akamtolee sadaka ya kuchinja ambaye nia IBRAHIM kwa mimi napendekeza mabadiliko yawepo kama katiba ya ilivyokuwa naviraka basi swala hili lina kiraka parekebishwe kama wakristo wamekuwa watulivu kwa muda wote huu basi waiislam wajalibu kuwa watulivu kama inashindikana basikama kijana akioa ujenga nyumba yake na kuanza kujitegemea na mkewe basi imani hizi kila moja ijitegemee mimi kama mpagani imani yangu ya kipagani inasema hiviunapochinja usikubali mnyama roho yake ikaishie mikononi mwako maana yake kata shingo kama kuku ikafe pekee ikiwa inarukaruka mpaka huai ukaishe Hivyo basi mkristo chinjia wakristo wenzeko wanunue mwiislam chinja waiislam wenzako wanunue acha kutuzuga ndani yake kuna kitu mmebeba ambacho amtaki kusema si mkristo wala mwiislam acha zenu nyote waswahili wapemba mnajuana.

    ReplyDelete
  10. Aaah! Bwana ndugu na jirani zetu mna matazizo. Hivi jamani dini si zinafundisha amani? Mbona mwapenda choko choooook!

    ReplyDelete
  11. ewe muislimu wa kitanzania kuwa makini namaishasisi tunaishi nje ya nchi hatujui nani kachinja wewe umakazana mwisilamu achinje kama ni vibudu basi sisi tunakula hizo nyama kwanza nakuuliza kuku na nyama kwasasa zitoka nje unategemea nani anachinja kuwa na amani nanchi yako

    ReplyDelete
  12. TUSIWE WAJINGA AU WAPUMBAVU SISI WAISLAM NANI KAKWAMBIA NYAMA ZIMECHINJWA NA MUISLAM DUNIA NZIMA HUYO MUISLAM ANAWEZA CHINJA NGOMBE NGAPI KWA KISU KILA SIKU?

    LAZIMA TUJUE MPAKA UARABUNI KWA WAARABU WENYEWE WANAKULA NYAMA YANGOMBE ILIOCHINJWA ARGENTINA AU BRAZIL NDIO WAZALISHAJI SANA WA NYAMA DUNIANI MBONA WANAKULA NA HUKO KILA KITU NI UKRISTU? MPAKA POPO MPYA NI MUARGENTINA MBONA HAWAJAGOMEA NYAMA HIYO?

    TUACHE UPUMBAVU HUO NI KURUDISHA MAENDELEO NYUMA WOTE WANAOJIHUSISHA NA MALUMBANO HAYO NI WATU AMBAO HAWAKENDA SHULE WALA HAWANA ELIMU

    ReplyDelete
  13. Very sad, it does not make sense. Kwa watu tunaoishi nje ya tanzania, inashangaza. Swala la nani achinje, jamani.Naomba waislam tunaoishi nchi za nje tuseme, nyama tunazonunua, ziko marked na price, expiring date. Aaaaah sijaona lable ya nani kachinja. Tunakula nyama na sijawahi kusikia mtu akiongelea. Sasa kwa nini tuvuruge amani ya nchi yetu. Hivi ni kwa sasa watu wengi nyumbani hawana kazi za kufanya au.Acheni kutumia dini kufanya upumbavu! At the same time hatuwezi kulazimisha wakristo kula nyama alivyochinja muislam. That's the fact. But hata sidhani wakristo wa shida na hili! Peace please

    ReplyDelete
  14. Conflict of interest ama Mgogoro wa Maslahi:

    Ndio suala kubwa ktk Siasa za Uchinjaji!

    Kama Mdau wa nne anavyosema, bidhaa hizo 5 kuwa mali ya Mchinjaji, pia Wadau wanaosema ni Uchoyo ili wengine wasile.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...