Ligi Daraja la Pili mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora imemalizika leo kwa timu tatu za Red Coast,  Abajalo na Friends Rangers zimefuzu kucheza hatua ya Kanda.
Katika mechi iliyochezwa Makurumla, Friends Rangers iliifunga Sharif Stars mabao 2-0. Mabao hayo yamefungwa na Khatib Kuduku katika dakika ya 12 na Mwenda Athuman katika dakika ya 57.Kwa matokeo hayo Rangers imefikisha pointi 8.
Kwenye uwanja wa Kinesi Red Coast wameibuka na  ushindi wa bao 1-0.Bao hilo limefungwa dakika ya 32 na Rafael Mapunda. Kwa matokeo hayo Red Coast wamefuzu hatua hiyo kwa kujikusanyia pointi 11 wakiwa vinara wa ligi hiyo.
Abajalo nao wamefuzu hatua hiyo baada ya kuichapacha Boom FC mabao 2-0. Hata hivyo mechi hiyo ilivunjika kutokana na wachezaji watatu wa Boom FC kutolewa kwa kadi nyekundu.Abajalo imeweza kufuzu baada ya kujikusanyia pointi 10.
Imetolewa na Ofisa Habari wa DRFA
MOHAMED MHARIZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...