NduguWaTanzania,
Kwa Niaba
ya TAWI la Chama Cha Mapinduzi Uingereza ,na kwa niaba yangu binafsi, Napenda kutoa
salamu za dhati kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho
Kikwete, kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein, kwa Serikali ya
Jamhuriya Muungano wa Tanzania,na kwa WaTanzania wote kwa ujumla kwa kutimiza miaka
49 ya Muungano wa nchi yetu, TANZANIA.
Pamoja na
salamu hizo, binafsi na kwaniaba ya wana CCM UK ,napenda kuwaomba na kuwakumbusha
WaTanzania wenzangu, tuendelee kuuenzi na kuulinda Muungano wetu kwa kudumisha
AMANI, UPENDO, UMOJA, UTULIVU na MSHIKAMANO. Hizi ndizo silaha zilizoweza kuulinda
Muungano huu ambao umetuletea Heshima ya kipekee Duniani kote, kwa takriban nusu
karne sasa.
Ndugu WaTanzania, nawasihi kamwe tusichezee amani tuliyonayo.
Tujifunze kutoka nch mbalimbali duniani ambazo wamechezea amani yao na sasa wamo ndani ya dimbwi
kubwa la machafuko, mauaji ya halaiki na yanayoendelea kila kukicha. Maelfu ya raia wasio na hatia wamepoteza maisha
yao katika Nchi mbalimbali, wengine kupata ulemavu wa kudumu, kupoteza makazi na
kuharibikiwa na mwenendo mzima wa mfumo wa maisha yao, milipuko ya mabomu isiyoisha
na raia kukosa amani na utulivu. WaTanzania kamwe tusikubali kuipoteza amani yetu kwa uchochezi wa watu wachache,
na ambao kwa sababu zao binafsi hawatutakii mema , na mpaka wako tayari kutumia
visingizio kama vya siasa na dini ili watusambaratishe.
Aidha,
WaTanzania wa Nje ya Nchi (Diaspora)tunajivunia na kutambua kwamba tuna nafasi ya
pekee ya kuchangia katika maendeleo ya Nchi yetu Tanzania katika Nyanja tofauti .
Mojawapo ya Mchango wetu Mkubwa kwa Taifa ni kufuatilia kwa ukaribu mambo
yanayoendelea nyumbani ,nakutoa mchango wetu wa kimawazo pale inapobidi.
CCM-UK tutaendelea
kutoa shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhur iya Muunganowa
Tanzania Dr.JakayaMrishoKikwete ,
pamoja na Serikali yake anayoiongoza kwa kuona umuhimu wa kutushirikisha
WanaDiaspora na kuthamini mchango wetu.Tunafarijika sana na kuahidi siku zote
kwamba tutaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Tanzania, kama
inavyowezekana kwa raia wengine
Weng
Ulimwenguni wanaoishi nje ya Nchi zao na wanachangia kukuza uchumi na
kuendeleza jamii zao kwa kutumia ujuzi na ufanisi waliojifunza ughaibuni.
MWISHO WaTanzania
wenzangu, tusherehekee sikukuu ya Muungano wetu kwa Amani na Utulivu,
tuvumiliane na sote tutie nia ya kudumisha na kuulinda Muungano wetu na kuwapuuza
wale wote wasioutakia wema Muungano wetu.
Tuwaenzi
waasisi wetu Baba waTaifa Hayati Mwl.
Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuulinda
Muungano, kudumisha amani na utulivu, aidha kufanya kazi kwa juhudi na kuinua uchumi
wa nchi yetu hadi kufikia azma ya - MAISHA
BORA KWA KILA MTANZANIA, SI NDOTO YANAWEZEKANA.
Kwa Niabaya
CCM UK – Nawatakia WaTanzania
wote popote pale walipo Dunian iMaadhimisho na Sherehe njema za siku hii adhimu.
MUNGU
IBARIKI AFRIKA - MUNGU IBARIKI TANZANIA
KIDUMU
CHAMA CHA MAPINDUZI.
-----------------------------------------------------
Mariam A. Mungula
KATIBU
CHAMA CHA MAPINDUZI – UINGEREZA
IMETOLEWA NA IDARA YA ITIKADI, SIASA NA UENEZI – CCM-UK
HATUTAKI MUUNGANO HATUTAKI MUUNGANO SHEREHEKENI WENYEWE
ReplyDeleteMungano ni NDOA YA MKEKA HAUFI NG'OOO!
ReplyDeleteKAMA HUTAKI HAMIA OMANI!
IT's too late!
ReplyDeleteMtoa Maoni wa kwanza anony wa Sat Apr 27, 12:18:00 am 2013
Gari imeshika kasi na sasa watu wanaangalia MUUNGANO WA UMOJA WA AFRIKA YA MSAHARIKI, kitu ambacho ni ndoto mawazo yako kuwa ya kuvunjika Muungano ndio kwanza unaimarika zaidi ktk AFRIKA YA MASHARIKI.
Chukua jembe ukalime ama chukua nyavu ukavue samaki kama huna kazi!