Mh.Balozi Ramadhan Mwinyi ndiyo alikuwa mgeni mharikwa katika sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika jijini New York. Sherehe hiyo ilihudhiliwa na watanzania wengi kutoka katika miji ya jilani na New York kama New Jersey, Delaware, Massachusetts na Connecticut. Watanzania waliungana kwa pamoja kwa kula chakula na kucheza music sambamba na vinywaji baridi.
Katibu wa jumuiya ya watanzania New York bwana Shaban Mseba akisoma risala katika sherehe hizo za muungano
Mwenyekiti wa jumuiya Hajji Khamis akiongea machache mbele ya watanzania waliojitokaza katika sherehe hizo zilizofanyika New York katika kitongoji cha New Rochelle.
Dr Chemponda alikuwa nae kama anavyoonekana katika picha akiongea machache juu ya jinsi gani anavyo ujua muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mama Ashura Duale nae anaujua sana muungano wa Tanganyika na Zanzibar na alikuwa mmoja ya washuhuda wa uchanganyaji mchanga wa pande zote mbili za Tanganyika na Zanzibar
Hii ndiyo cake ya muungano ikiwa mezani
Ukodak wa pamoja katia ya Dr Chemponda, kushoto mama Ashura katikati, na kushoto kwa mama Ashura ni mama mwenye nyumba wa Mh. Balozi Mwinyi, Na kulia na Mh. Balozi Mwinyi
Ukodak mbele ya cake 
Mh. Balozi akikata Cake tayari kwa kuwalisha wana muungano walio jitokeza katika sherehe hizo
Mh. Balozi Ramadhani Mwinyi akimrisha kipande cha cake mama mwenye nyumba wake kabla ya watu wengine awajapata nafasi hiyo. Kwa picha zaidi ya sherehe hizo zilizofanyika katika jiji la New york bofya read more.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Waswahili wa Marekani mnajua kusherehekea. Nilipo mimi hakuna kitu wala waswahili hatuonani. Hata mtu akifiwa ukiwapigia jamaa wanasema they are busy - strange countrymen here. Nawapongeza nyie kwa ushirikiano mlio nao.

    ReplyDelete
  2. POLE SANA KAKA AU DADA MAANA HUJASEMA WEWE NI NANI NA UKO WAPI. EBU TUWEKE WAZI UKO NCHI GANI AMBAYO HAINA WABONGO TUKUELEKEZE WAPI UTAPATA UHONDO HUUUU ANGALAU HATA KWA NCHI JIRANI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...