Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania nchini Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo (pichani) anayofuraha kubwa kuwakaribisha watanzania na marafiki wa Tanzania kutoka pembe mbali mbali za Dunia katika maadhimisho ya Sherehe Ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani, zitakazofanyika mjini Koloni hapa ujerumani.siku ya juma mosi Tarehe 27.04.13 kuanzia saa :08:00 za mchana hadi usiku wa manane.
Katika sherehe hio ambayo imedhaminiwa na Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushirikiana na culture center ya sarakasi. Die Zirkus Fabrik, kutakuwa na maonyesho ya bidhaa za Tanzania, na atakayependa anaweza pia kununua bidhaa hizo. Ngoma za asili kutoka Tanzania, Mwanamuziki Kongwe Bi.Tabia Mwanjelwa naye atakuwepo, Msanii wa Bongo Flava Shah Smooth mwenye maskani yake Dublin,. Kikundi cha Sarakasi kitafanya mavitu yake Live ! na mwisho watanzania na wageni wote watapata Fursa ya Kuduarika na midundo kutoka Tanzania kupitia DJ Sudi Mnete wa DW.
Akihojiwa na vyanzo vyetu vya habari mwenyekiti Bw Mfundo Alisema, Madhumuni ya sherehe hiyo sio tu kusherehekea siku kuu ya muungano pekee, bali ni kutimiza moja ya maazimio ya UTU la kuwakutanisha Watanzania wanaoishi nchini humo na kutangaza utamaduni wetu wa Tanzania kwa wenyeji wetu hapa Ulaya. Aliendelea kufafanua kwamba moja ya Agenda ya UTU ni kuhakikisha Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani wanakuwa pamoja kwa hali zote, wanashirikiana kwa karibu na kusaidiana. Aidha pia kuhakikisha wasanii wanaoisha hapa ujerumani wanatangaza kazi zao hadharani na wanazitumia kazi hizo kujipatia manufaa zaidi.Hivyo katika sherehe hii (UTU) imealika wasanii mbali mbali kuja kuonyesha kazi zao. Mwenyekiti alimaliza kwa kuwashukuru wasanii na watanzania ambao tayari wameshajiandikisha kushiriki katika sherehe hiyo kubwa Mjini Koloni,
Umoja ni Nguvu!
KARIBUNI SANA MJINI KOLONI
Muungano wa Tanzania bara na visiwani?!
ReplyDeleteWewe Mtoa maoni wa kwanza, unaonyesha sio Mtanzania ama hukusoma ktk Mtaala wa Elimu ya Tanzania, sasa ulitaka uwe Muungano wa Tanzania bara na wapi ?, na Burundi ulipotokea wewe?
ReplyDeleteHujui Tanzania ni Muungano wa Tanganyika(Bara) na Zanzibar na Pemba (Visiwani)?
Ninyi ndio wapinga Muungano wenyewe kutokana na uulizaji wako wa swali.
UTU huko Ujerumani, ktk mchakato wa maadhimisho ya Sherehe za Muungano huko Mjini Cologne msisahau vitu hivi muhimu:
ReplyDelete1.Mashairi,Maigizo na ngonjera,
Muandae ya kuwananga Mamluki na Wapinga Muungano ambao wengi wao waliopo huko Majuu si Watanzania tena wameshapoteza Uraia na sasa ni wabeba Maboxi na Wakimbizi.
Muandae Mchezo unaoonyesha Jinsi Mapinduzi yalivyo fanyika Zanzibar Januari 1964 (huku Mkoloni wa KIARABU akipinduliwa) na halafu mwezi April-1964 ukafuatia Muungano.
2.Watanzania safi na Wanamapinduzi, muandae NYUNDO na JEMBE za chuma kama alama ktk eneo la sherehe ili Wapinga Muungano waone wakileta ujinga nyundo itawashukia vichwani utosini !!!