FOWARD MOTION ikishirikiana na Dorctor's Plaza Heart Clinic pamoja na Lancet Laboratories wamezindua mpango wa  upimaji afya (Medical checkup) mwishoni mwa juma katika makao makuu ya  Doctor's Plaza Heart Clinic yaliyopo Sea View jijini Dar es salaam. 
Katika siku hii  washirika hao walitoa huduma ya bure ya upimaji wa Cholestrol, Sugar, Blood Pressure, ECG na BMI. Waalikwa wote walipata fursa ya kupima vipimo hivyo na kupata ushauri wa bure (free consultation) kutoka kwa madaktari Bingwa Campaign hiyo pia iliambnatana na mafunzo mbalimbali ya afya kutoka kwa mabingwa hao.
Kwa mujibu wa msemaji wa DPHC, Bi Sofia Byanaku,  Mpango huo endelevu, utaendelezwa kwa njia tofauti na ngazi tofauti, akisisitiza kuwa Kinga ni bora kuliko Tiba!
 Wadau wakisikiliza maelezo toka kwa madaktari kuhusu umuhimu wa kupima afya
 Dkt Masatu akitoa elimu ya bure kuhusu umuhimu wa watu kupima afya zao
Dkt Vivian mlawi akitoa ushauri kwa Nancy Sumary aliyekuwa mmoja wa wadau waliofika kupata huduma hiyo ya bure ya kupimwa afya na kupewa ushauri

 wadau wakisubiri zamu kupimwa
Nesi akimpima bloga maarufu Missie Popular

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Toa maelekezo sahihi ilipo, hujui biashara matangazo.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...