Balozi wa Tanzania nchini China
Philip Marmo akiongea na mwekezaji Zhou Yi (wa pili kushoto) ofisini kwake
jijini Beijing China. Wengine katika picha ni Pan Lei, Mkurugenzi wa Kampuni ya
kichina ya Fashion Tourism yenye ofisi yake nchini pamoja na Allen Lee kutoka
Chama cha Mawakala wa Utalii Beijing, China. (Picha na Pascal Shelutete wa
TANAPA)
Mwekezaji wa China Zhou Yi |
Na Pascal Shelutete
Milionea wa kutoka Jamhuri ya
Watu wa China Zhou Yi anatarajia kujenga loji kubwa ya kisasa katika Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti. Zhou alisema hayo jana jijini Beijing nchini china alipokutana
na ujumbe wa serikali ya Tanzania unaotembelea China kwa lengo la kutangaza
utalii na kutafuta wawekezaji katika sekta ya utalii nchini.
Zhou anamiliki mtandao wa
makampuni tanzu yanayofahamika kama Hengxu Group of Companies yenye makao makuu
yake katika mji wa viwanda wa Sichuan na ameajiri watu zaidi ya 7,000 na ana
mtaji wa zaidi ya dola za kimarekani milioni mia saba alisema kuwa alitembelea
hifadhi ya Serengeti mwezi Machi mwaka huu na kuvutiwa sana na uzuri wa uasili uliopo Serengeti.
Alisema kuwa hivi sasa yuko
katika hatua za awali ya kuomba kupatiwa eneo la kuwekeza ambapo ujumbe wa
serikali unaoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi.
Nuru Millao ulimuhakikishia upatikanaji wa eneo hilo ili kupunguza tatizo la
uhaba wa vitanda kwa wageni nchini.
Ujumbe wa Tanzania uko nchini
China kuhudhuria maonyesho maarufu ya utalii ya COTMM katika jiji la Beijing
pamoja na kuandaa semina kwa wawekezaji wa China na Wamiliki wa kampuni za
Utalii kuhusu vivutio vya utalii nchini pamoja na kuainisha fursa zilizopo za
uwekezaji katika sekta ya utalii nchini. Semina hizi zinazofanyika katika miji
ya Shanghai, Beijing na Guangzhou zinalenga kuongeza idadi ya watalii na
wawekezaji kutoka China nchini.
Jijini Beijing emina hizi
ilivutia idadi kubwa ya wawekezaji ambao walihamasika hasa kutokana na fursa
zilizopo katika maeneo yaliyohifadhiwa nchini. Wengi waliamua kutembelea
Tanzania kaika siku za usoni ili kuona maeneo watakayoamua kuwekeza.
Mapema Balozi wa Tanzania nchini
China na Bi. Millao waliwahakikishia washiriki kuwa Tanzania ni eneo zuri
kuwekeza kwa sasa hasa kwa kuwa na vivutio vingi ikiwa ni nchi ya pili duniani
baada ya Brazil. Aidha, wawekezaji hao walihamasishwa kuchangamkia fursa
zilizopo hasa kutokana na utulivu wa amani uliopo nchini.
Sio mbaya lakini hao jamaa siwaamini kabisa ...wanapenda sana kula wanyama mbalimbali....msije mkastuka mbuga nye
ReplyDeleteI think that is a very wrong approach. The bed capacity within Serengeti ecosystem is more than enough unless we want to spoil "the goose that lays the golden eggs" and engage in mass tourism like our neighbors in the north. Such ivestments should be directed to Katavi National Park for diversification and opening up other new tourism products. We should put to maximum use the Songwe International Airport in Mbeya as the hub to SADC region and link to Mpanda as well as Copper belt in Zambia. I am proposing a tourist circutit linking Nsumbu National Park on Lake Tanganyika shores in Zambia to Mahale, Katavi, Kitulo and Ruaha national parks. The market is unexplored and that is where the Chinese investments should be directed.
ReplyDeleteHapo ni kumkabidhi panga mwendawazimu..wachina wanatumia pembe za ndovu na pembe za rhino na mifupa ya chui kama dawa...si mmempa shamba huyo akavune. tunahitaji wawekezaji lakini sharti tuangalie na sifa za wawekezaji sio hela tu...
ReplyDeleteThe Chinese have arrived in Serengeti!
ReplyDeleteThe Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!
The Chinese have arrived in Serengeti!