Tamasha la Airtel Yatosha lenye lengo la kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali za Airtel ikiwemo huduma mpya ya Airtel Yatosha linalofanyika katika mikoa mbalimbali nchini mwishoni mwa wiki hii litafanyika katika mkoa wa Pwani.

Shangwe za Airtel yatosha litajumuisha wasanii mbalimbali nchini wakiwemo Ney wa Mitego, sir Juma Nature, kikundi cha Tip top connection kikiongozwa na madii, msanii wakizazi kipya Roma Mkatoliki pamoja na burudani nyingi toka kwa wasanii chipukizi na burudani za dansi na acrobatic kutoka katika kikundi cha vinoko.


Tunawakaribisha watanzania na wakazi wa mkoa wa pwani kuhudhuria tamasha ili siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 13 na 14 mwenzi wa 4, katika viwanja vya sokoni chalinze, kuanzia saa tatu mpaka saa kumi na mbili jioni.


Kiingilio ni BURE, njoo na kitambulisho chako usajili namba yako na kuunganishwa na huduma poa ya Airtel yatosha na kupata ofa kibao kutoka Airtel.

Airtel itaendelea na burdani hizi za shangwe katika mikoa mingine katika kuitambulisha kwa wateja wake na watanzania huduma ya Airtel Yatosha inayomuwezesha mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.

Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99#

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...