Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa wa kwanza kushoto akisaini mkataba wa makubaliano ya mkopo wenye riba nafuu kwajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kulia ni Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada akitia saini pia makubaliano hayo.
Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akibadilishana hati za makubaliano ya mkataba na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada, mkataba huo utaiwezesha Tanzania kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akisisitiza jambo wakati akiwa na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada mara baada ya kukamilika kwa shughuli za utiliaji saini wa makubaliaono ya mkopo wa riba nafuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Miongoni mwa mambo nililofurahisha katika habari hii ni ile niliosikia kwenye magazeti kwa mapitio ya redioni kuwa, baada ya makubaliano hayo waziri wa Tanzania aliongea na Watanzania kwa kiingereza na Balozi wa Japan aliongea na Watanzania kwa KISWAHILI. Nimependa somo hilo!

    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...