Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Zanzibar, Mhe Haroun Ali Suleiman,akimkabidhi fedha taslima
zaidi ya shilingi Milioni tatu, mmoja wa
viongozi wa shehia ya Mzuri kwa ajili ya mashindano ya kumuenzi aliyekuwa
kiongozi wa siku nyingi nchini marehemu Hasnou Makame
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi naUshirika Mhe Haroun Ali Suleiman akizungumza
na Balozi mdogo wa India hapa nchini Mhe Pawal Kumar ofisini kwakwe Mwanakwerekwe
mjini Zanzibar, jinsi India itakavyoweza kuisaidia Zanzibar juu ya kuanzishwa kwa Benki ya Jamii.
![]() |
Wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari wakipata maelezo kwa Mshauri Mkuu wa Msafara wa wakandarasi kutoka India Bw. Ummashan Kar Misra juu ya kukifanyia matengenezo kiwanda cha sukari Mahonda |
Kondakta
wa gari ya abiria ya Chwaka akiondoa marembo ya mbele ambayo yanamzua dereva
kuona mbele baada ya kuamriwa kufanya hivyo na Askari wa Usalama Barabarani
katika uperesheni wa ukaguzi wa Magari ulioandaliwa na Idara ya Usafiri na
Lesseni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya
usalama barabarani.
Picha zote na Khamisuu Abdallah wa Globu ya Jamii, Unguja
tofauti ya bara na zanzibar, zanzibar umekosea unapewa nafasi ya kurekebisha kosa, bara umekosea unapigwa faini, mradi umewalipa pesa yao hata usiporekebisha kosa haiwahusu
ReplyDeleteNi vema mmeliona hilo kwani hata mimi nipandapo basi huwa nakerwa sana na hayo mapambo mengi kwenye kioo cha dereva ambayo humzuia hata dereva sione mbele vizuri
ReplyDelete