Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM kwenye uwanja a shule ya Msingi Gairo B, mjini Gairo mkoani Morogoro leo hii.

==========  ========  ========

NA BASHIR NKOROMO, GAIRO.

 CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kukerwa kwake na matukio ya kejeli matusi na uvunjifu wa amani yanayoanza kushamiri bungeni  na kusema kuwa matukio hayo ni dhihaka ya hali ya juu inayofanywa na wabunge dhidi ya wananchi waliowachagua.

 Hayo yalisemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa shule ya Msingi, Gairo mkoani hapa, Aprili 18, 2013, ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

 ” Mambo haya yanayofanywa na wabunge  kama ilivyotokea jana (juzi), ni dhihaka inayofanywa na wabunge kwa wanancjhi waliowachagua. Baadhi ya wabunge wanafanya vituko hivi huku wakiwa wanatambua wazi kwamba heshima waliyopewa ni kwenda bungeni kujadili matatizo ya wananchi ambayo ni mengi kama migogoro ya ardhi. Hili tukio la jana ni  aibu ya mwaka”, alisema Nape.

 Alisema, muda wanaokuwepo bungeni, wabunge wanapaswa kuutumia wote kwa hekima busara na uwezo wao wote kujadili namna ya kuwezesha Watanzania kufikia maisha bora na siyo kuutumia muda huo kujadili tofauti zao za kisiasa au namna ya kutekeleza malengo yao binafsi ya vyama vyao.

 ”Hatua hii ya wabunge wa Chadema kuamua kuzusha tafrani na kuvunja kanuni za bunge kwa makusudi ni ya hatari sana, hivyo wananchi wanapswa kujifunza kwamba hawa siyo watu wa kuwapa madaraka. Tazama hivi sasa bungeni wapo wachache sasa wananchi wakihadaika wakawachagua na kuwa wengi bungeni patakuwaje? Hili ni fundisho tosha”. alisema Nape.

 Alisema, hatua ya Wabunge na viongozi wa Chadema kulijadili suala la Mkurugenzi wa Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare kuhusiana na ugaidi huku wakijua kwamba ni suala ambalo lipo mahakamani, ni la kujaribu kuingilia uhuru wa mahakama kwa makusudi ili ifikie mahala mahakama itupilia mbali kesi hiyo kwa kigezo cha kuinngiliwa uhuru wake.

 ”Haya ni matumzi mabaya ya bunge ambayo yanasukumwa na viongozi wao ikiwemo kuingilia uhuru wa mahakama, ili hatimaye ionekane uhuru wa mahakama umengiliwa kuhusiana na kesi hiyo na hatimaye itupiliwe mbali. Kila mwenye akili anajua kwamba  huu ni mkakati malum wa Chadema”, alisema Nape.

 Mbali na kukizungumzia bungeni suala ya Lwakatare, Chadema wamekuwa wakilisema pia mitaani, akitoa mfano hatua ya hivi karibu ya Mbunge wa Singida, Tuntu Lissu kufanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo na kwamba mbali na kutafuta kesi hiyo itupwe pia ni juhudi za Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama. Bofya hapa kwa habari kamili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MIMI SASA CHADEMA WANANIKERA SANA, NIMEJARIBU KUFUATILIA SIASA ZA NJE NIMEGUNDUA KUWA CHADEMA NI PANDIKIZI LA UMWAGAJI DAMU TANZANIA. WASOMI WANAZUONI NA WANANCHI WOTE TUFUNGUKE MACHO SASA. MIMI SINA CHAMA ILA NILIPENDEZWA NA MWANZO WA CHADEMA LAKINI SASA WANAONESHA WAZI WAMETUMWA NA WATU FULANI KUIHARIBU TZ ILI WATU HAO WAJE IBA SANA TZ. HONGERA CUF, NCCR MAGEUZI, CCM NA VYAMA VINGINE. SISI TULIOPO HUKU UGAIBUNI TUNAFATILIA MOVEMENT ZENU.

    ReplyDelete
  2. Kumbe nyie wa ughaibuni hamjui kitu...Hapa tz ni kuchuana tu kwa vyama. wote ccm chadema ni vita kwa kwenda mbele kila chama kinataka madaraka... sisi yetu macho..

    ReplyDelete
  3. Nape ulianza vizuri lakini ulipoanza kuishambulia CHADEMA peke yake nikaacha na kusoma habari yenyewe.Kwa ufupi ni bahadhi ya wabunge kutoka vyama vyote vya siasa walioko bungeni.Nape usitufanye kama sisi hatufuatilii Bunge.Na kuna bahadhi ya wagunge kutoka pande zote wana busara kweli kweli wanajaribu kutuliza hali,wana maneno ya hekima.Tatizo liko kwa wale wanaoongoza bunge.Limewashinda acha kuzungukazunguka NAPE.Bunge la vyama vingi lina tofauti sana na Bunge la chama kimoja

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...