Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akiwapungia maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo kwenye sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Kasarani,jijini Nairobi Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete,Mabalozi na watu wengine mbalimbali.Picha zote kwa hisani ya Mike Kariuki wa Capital FM.
Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akisoma hotuba yake mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo kwenye sherehe iliyofanyika ndani ya uwanja wa Kasarani,Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais wa nchi mbalimbali ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria.
 Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Makamu wake William Ruto.
 Rais Uhuru Kenyatta akila kiapo cha Urais,kuwa rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe zilizofana kwa kiasi kikubwa ndani ya uwanja wa kasalani.
 Rais wa Uganda,Mh Yoweri Kaguta Museven akisoma hotuba yake fupi wakati wa kuapishwa kwa Rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe zilizofanyika ndani ya uwanja wa Kasalani,jijini Nairobi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tuwekee comparison na Kiapo cha Moi mwaka 2007

    ReplyDelete
  2. Kwanini mnachanganya matumizi ya herufi "L' na 'R", ankal mara nyingi waandishi wetu hawako makini wanapotamka au kuandika neno Kujiuzulu wanasema Kujiuzuru, au kama ulivyosema hapo ankal KASALANI badala ya KASARANI. Je hiyo ni effect ya mother tongue au overdose ya Kiswahili?

    ReplyDelete
  3. This is not fare michuzi ongeza picha

    ReplyDelete
  4. watanzania mngeijua histori ya chaliiiiii mngeshanga mafisadi daima wanakwenda mbele

    ReplyDelete
  5. Shule jamani!, THIS IS NOT FAIR siyo 'this is not fare' kama huyo anonymous hapo juu.Walimu aheni mgomo na msipotoshe watoto au ninyi pia ni vilaza??????

    ReplyDelete
  6. Kaka Hapo Juu matumizi ya L & R nakuunga mkono kabisa yaani ni aibu kabisa kwa Waandishi wa habari ambao hushindwa kutofautisha L na R, wengine ni wanamuziki wa bongo fleva yaani wale ndo mwisho kabisa kwa kuharibu kiswahili.

    BAKITA mko wapi!!

    Mlomry

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...