Kamanda  wa polisi  wa mkoa  wa Mbeya  Diwani Athuman
.............................................................

Taarifa  kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai  kuwa hali  si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa  vurugu kubwa zinazodaiwa kusababishwa na masuala ya  kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam .

Habari zinasema vurugu  hizo zimeanza  majira ya saa nne asubuhi  kwa makundi  ya vijana  kuandamana mitaani na kuvutana  kuhusu uamuzi  wa viongozi  wa dini ya kikristo Tunduma  kuandika barua kwa mkuu  wa wilaya  kutaka  kuruhusiwa kuchinja  wakati wa Pasaka.

Insemekana kuwa kabla ya  Ijumaa kuu  viongozi hao  wa dini ya Kikristo  walikutana na mkuu  wa  wilaya  Mhe. Momba Abuud Saidea ambae  aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya  kufanya hivyo .

Hata hivyo inaelezwa  kuwa  vurugu  hizo za  leo hazina mahusiamo ya moja kwa moja na masuala ya dini kwani  wanaoshiriki katika  vurugu  hizo ni vijana  wapiga debe ambao baadhi yao  wamechanganyika na  vibaka  kwa lengo la kuchafua hali ya hewa, kwani  suala la uchinjaji ambalo lilifanyika  siku ya Pasaka  halikuwa na mvutano  wowote baada ya wakristo kuchinja katika bucha zao na  waislamu hao  kuchinja katika mabucha yao na kila mmoja  kufanya biashara  kwa kupata  wateja wake kama kawaida .

Ila katika hali ya kushangaza ni baada ya  leo kuibuka  kundi hilo la  vijana  wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbali mbali kuanzisha vurugu kiasi cha  polisi  kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya  wananchi  waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali .

Kutokana na vurugu  hizo mpaka  wa Tunduma  ambao unaingia nchi  za kusini  wa Tanzania  ulifungwa  pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka  Sumbawanga  pia  kuzuiwa  kuendelea na  safari hadi hali  hiyo  ilipotulia mida hii saa 8 mchana baada ya kamanda wa polisi wa mkoa  wa Mbeya  Diwani Athuman  kufika  eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Sisi wakristo aka wamisionari,nikiwa mdogo wazazi wakinunua kitoweo cha kuku, au wakati wa pasaka au noeli mbuzi, basi jirani yetu muislamu aka mwana zuoni,tutamuomba aje kuchinja, kwani sisi tulikuwa hatuna noma, sababu washikaji zangu kina abdallah, athumani, shabani wanaweza nao kuzuka nyumbani baada ya kucheza cha ndimu ili wapate "MMANGO" sote tukamanga, sikuhizi vurugu tupu, upendo wa zamani umeishia wapi?

    ReplyDelete
  2. upendo wame na wanauondoa wao! ni bahati mbaya sana kwamba badala ya kuendelea kuwapenda na kuwavumilia, na sisi tunajifunza kuwa kama wao!!

    ReplyDelete
  3. kwa nini wasiruhusiwe kuchinja?

    uzuri ni uwazi, kutakuwa hakuna kula kwenye nyumba za dini nyengine iwe harusi, kilio, au laa.

    ReplyDelete
  4. upendo wameondoa CHADEMA na baadhi ya viongozi wa dini wanaochochea fujo

    ReplyDelete
  5. Swala la nyama linahitaji busara isiyo ya kawaida.Hili linaweza kulipua nchi katika vipande vipande maana linagusa imani zetu.Wakristo hawana shida kula nyama iliyochinjwa na waislam/wasio na dini au wakristo wenzao tatizo hilo halipo.Tatizo lipo kwa waislam ambao pamoja na mambo mengine wao wanawaona wakristo kama "makafri" hawafai kuchinja nyama si kwasababu nyingine yoyote bali kwasbabu mafundisho yao wanavyodai kuwa ni makafri" na kwa wakristo wana haki sawa kama wengine na uwezo wa kuchinja wanao sasa hapa ndipo biashara inaponoga.Mkuu wa kaya hana maamuzi amebaki maneno matupu.sasa sijui

    ReplyDelete
  6. wana "filosofia" walisema YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOME TIME, BUT CAN'T FOOL THE PEOPLE ALL THE TIME. Kwa maana hiyo, kizazi cha sasa kila upande umegundua hilo lakini kuna upande mmoja ambao umedhulumiwa zaidi, na ule uliodhulumu unajitahidi kupata mashiko ya kuendelea kuhakikisha unaendeleza dhuluma za tangu mwanzo. KUMBUKENI kizazi kipya hakijua habari ya kuvumiliana. SERIKALI IKIKAA KUSHUHULIKIA UPANDE MMOJA KWA VITENDO NA MWINGINE KWA MANENO, Basi tunaelekea tutafuta kuheshimiana kwa STYLE ya Rwanda 1994. na safari hiyo ya rwanda imeanza basi ndio tumeondoka ubungo kuitafuta Dom, Sgd, kahama Kagera kabla ya kufika KIGALI. WATANZANIA WA SASA TUMESHAPOTEZA MAMBO 3. UPENDO, KUSHIRIKIANA NA KUVUMILIANA. na kwa sehemu kubwa serikali imechangia kwa kukumbatia UPANDE mmoja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...