Jengo moja la ghorofa nane linalosemekana lilikuwa likijengwa kinyume cha sheria limeporomoka na kuua watu 47 na kujeruhi wengine 70 jijini Mumbai, India siku ya Alhamisi jioni. 

Waokoaji wakiwa na nyundo, misumeno, jeki na bulldozer zipatazo sita walikuwa wakijitahidi kunasua walionasa kwenye jengo hilo lililo maeneo yam situ liiltwalo Thane.

 “Kuna uwezekano kuna watu wamenasa katika kifusi” Kamishna wa Polisi wa eneo hilo Bw. K.P. Raghuyanshi amesema leo mchana. 

Wakati linaporomoka inasemekana ndani ya jengo hilo mlikuwa na watu kati ya 100 na 150, wengi wakiwa ni wakazi wa humo mjengoni na wengine wajenzi. Zaidi ya watu 20 hawajulikani walipo hadi sasa, kwa mujibu wa Bw. R.S. Rajesh, afusa wa kitengo cha majanga na uokoaji. Waliokufa ni pamoja na watoto 17. 

Ghorofa nne za jengo hilo zilikuwa zimeshamalizika kujengwa na watu walikuwa wanaishi humo, ambapo wajenzi walikuwa wakimalizia ghorofa zingine tatu na walikuwa katika kuongezea ya nane ndipo lilipobumburuka.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Yale yaleee...nchi zote zenye corruption zinakumbwa na haya majanga yanayosababishwa na wanadamu. Sasa tumeng'ang'ania kuwa tatizo liko Dar es Salaam je huko mikoani Arusha, Mwanza, Mbeya, Moshi na kwingineko kuna usalama gani?

    ReplyDelete
  2. Nchi ambazo uti wa mgongo wa uchumi ni rushwa.

    ReplyDelete
  3. Kikwangua roho kikingine hicho nacho chatesa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...