Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Abdallah Hemedy(kulia)akifuatilia moja ya namba ya simu ya mshindi wa Promosheni ya"MAHELA" inayooneshwa na Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(katikati) Mshindi huyo aliejishindia kitita cha shilingi Milioni Tano,ni Bw.Kibwana Kitogo ambae ni mkazi wa Handeni Tanga,anaeshuhudia kushoto ni Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael. Zaidi ya shilingi Milion 122 bado zinaendelea kushindaniwa,Mteja anatakiwa kutuma neno MAHELA kwenda namba 15544 ili aweze kujishindia fedha taslimu.
Meneja mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akifurahia jambo na bwana. Abdi Mkande (64) Mkazi wa Kitunda, Dar es Salaam, wakati wa makabidhiano ya fedha alizoshinda kupitia promosheni ya MAHELA, inayoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania. Anayeshuhudia na Msaidizi wa Ofisa mkuu wa Biashara - M PESA, wa Vodacom Alice Lushiku.
Msaidizi wa Ofisa Mkuu wa kitengo cha biashara-M-PESA, Alice Lushiku (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa Promosheni ya Mahela Bi. Rose Furahisha, ( 61 ) mkazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam, aliejishindia shilingi milioni moja kupitia promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania. Anayeshuhudia ni Mume wa Bi. Rose bwana, Furahisha.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatiliajambo kwa umakini wakati wa kuchezesha Promosheni ya MAHELA inayoendeshwa na Vodacom Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Dadangu Alice, nadhani hii si mara ya kwanza kuwa infront of the camera. Una exposure ya kutosha, sikuona sababu na bado najiuliza kwanini umevaa such top kwenye pressconference.Ushauri tu kama mwanamke mwennzangu we do not were such nguo zinazoexpose makwapa, especially kwenye such event. Natumai utanielewa, that thing inakushusha trust me!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...