Katika tukio moja jijini Dar es Salaam katika Mtaa wa Indhira Ghandhi/Mshihiri, Tanki nne (4) za Maji za Lita 5000 kila moja zaanguka kutoka juu ya jengo la ghorofa 13 na kuvunja nyumba ya jirani.

Tanki hizo bado zilikuwa zinafungwa juu ya ghorofa hilo na mkandarasi alikuwa hajaweka vizuizi vya aina yoyote.

Naomba kuuliza wadau, matanki ya lita ngapi zinaruhusiwa kisheria kupandishwa juu ya maghorofa? na kwenya tukio kama hilo nani awajibiishwe, CRB, Mkandarasi, mmiliki wa jengo au…?

Kibao cha Mkandarasi wa Jengo hilo.

Tanki zote chaliiiiii
Sehemu ya Madhara yaliyotokea kwenye nyumba zilizopo jirani na Jengo hilo.
Hili ndio jengo lenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Bora ninyamaze maana upuuzi huu unatosha sasa

    ReplyDelete
  2. Jina mmoja katika kibao cha mradi wa ujenzi wa jengo hilo la ghorofa 13 nimeliona tena ktk ajali ya lile jengo la ghorofa 16!

    ReplyDelete
  3. Haya yanatokana na yale yale yaliyosababisha jingo la Ghorofa 16 kuanguka wiki chache zilizopita.

    1.KUTOKUFUATA KANUNI ZA KIKAZI.

    2.UKIUKWAJI WA TARATIBU ZA UJENZI.

    3.RUSHWA ILIYOKITHIRI.

    4.UJUAJI MWINGI KULIKO TAALUMA.

    5.HEBU ANGALIENI KTK BAO LA MKANDARASI HAO MAWAKALA KAMPUNI ZA UKANDARASI WANAOSHIRIKI WOTE NI KTK TUJUANE CO.LTD. , KWETU KUMOJA BUILDERS LTD. N.K (Hawakupatikana kwa vigenzo vya Ushindani yaani NCB(National Competitive Bidding), ICB (International Competitive Bidding)

    ReplyDelete
  4. Heeee Uhindini tena?

    Ghorofa 16 zimeanguka wiki 3 zilizopita leo tena Matenki ma 4 kutoka Ghorofa ya 16 chini!

    Wahindi wamezidi kuendesha mambo kiholela!

    ReplyDelete
  5. Hivi mpaka watu wangapi wafe?

    ReplyDelete
  6. Ni muhimu tuanze kutembea na Mahelmeti vichwani(Kofia za Chuma) ama Kuvaa Masanamu ya MICHELLIN mwilini ili kujikinga na maafa ya Maghorofa kuporomoka tunapokuwa matembezini ktk Mitaa ya Maghorofani tukiwa Jijini Dar.

    Wadau muwe mnaweka Mabanda ya Wateja kukodishia vifaa hivyo wakitokea makwao nje ya mji na wanapofika Jijini wanakodi.

    Mpo Wajasiriamali?

    ReplyDelete
  7. Kazi ipo mwaka huu inabidi Watanzani tuwe makini tunapopita karibu na hayo majengo marefu.

    ReplyDelete
  8. HAYA YOTE YA WATU KUNUNUA MATANKI YA LITA 10,000 AU 100,000 AU LITA 10 YASINGEKUWEPO KAMA VIONGOZI WENU WANGETUMIA MABILIONI YA MSAADA NA FEDHA ZA UMMA KUBORESHA MTANDAO WA MAJI SAFI KWA WALIOPIGA KURA NA SIYO KUNUNUA MASHANGINGI KIJIFAHARISHA.

    KWA WENYE ELIMU ZAO, MTU ANAYEWEKA TANGI LA MAJI ANGELAZIMIKA KUNUNUA KISUKUMA MAJI (WATER PUMP) KUPANDISHA MAJI TOKA CHINI NA SIYO KUTUNDIKA VITU VYA HATARI HUKO JUU.

    TABU YA KUWA NA WEZI WASIOKUWA NA ELIMU YA MAISHA NA KUISHI SALAMA. HAKUNA RISK ASSESSMENT KUZUIA AJALI KAMA HIYO ISITOKEE. MNAISHI KAMA WANYAMA. HATA MNYAMA KABLA HAJAFUNGA MBUGA, HUANGALIA SIIMBA AU YAO ANAHEMEA WAPI...WANACHAGUA NJIA NYINGINE KUWAEPUKA. TAMBARAREEEEEEEEE KUFENI TU NA RUSHWA ZENU.

    ReplyDelete
  9. Suleiman M. Mtoni (0769 535 349)
    Meneja-Afya, Usalama na Mazingira (Kampuni ya ujenzi ya Advent)
    Mkandarasi aliyepo kwenye kibao, hahusiki tena na jingo hilo. Mkataba wake na mwenye jengo ulikuwa kujenga fremu ya nnje na mpango wa vyumba ndani tuu. Baada ya kumaliza ujenzi wa mwanzo, mwenye jengo Ghadeer Developers (Mohamed Karmali kama anavyoonekana kwenye vibao vya ujenzi) alikabidhiwa jengo lake mwezi wa kumi mwaka 2012 kwa ajili ya kufanya kazi kumalizia (finishing) inafanywa na mkandarasi mwingine aitwaye Hong Yang International Company. Mpaka sasa kibao cha mkandarasi aliyepo “Advent” kipo hapo ili kuhakikisha kazi ya fremu ya nnje na mpango wa vyumba (main structure pekeyake) haipati kasoro yoyote ndani ya miezi sita inayoishia mwishoni mwa mwezi huu wa nne. Tunaomba waandishi wote mchukue tahadhari na kutafuta taarifa za kina kabla ya kutoa taarifa zozote kwa umma.

    Suleiman M. Mtoni (0769 535 349)
    Health, safety and Environment Manager-Advent Construction Ltd
    Advent is not on site any more. Our scope was construction of STRUCTURE ONLY which was handed over to the client in Oct 2012 and we demobilised immediately thereafter. All other works are being contracted and supervised by the owner Ghadeer Developers (Mohamed Karmali as the names of clients appears on the sign board). Our board is there only to cover defects liability period for STRUCTURE WORKS ONLY until April end 2013. Contractor on site is Hong Yang International Company. We request publishers to exercise caution before publishing misleading information or images.

    ReplyDelete
  10. Corruption ndo tatizo mama.

    watu hawafati kanuni kwani wanajuwa matatizo hutatuliwa kwa rushwa. They will always do away with any problem.

    yaani corruption ndo solution yetu.

    ReplyDelete
  11. Nimufurahia hiyo comment ya TUJUWANE LTD na KWETU KUMOJA LTD.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...