UONGOZI wa Yanga umewataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi kwenye mechi yao dhidi ya Coast Union siku ya Mei Mosi kushangilia kutawazwa rasmi mabigwa wapya wa Tanzania.

Yanga ambayo ina pointi 56 imebaikiza pointi moja kuwavua rasmi wapinzani wao Simba ubingwa wa Tanzania na kwamba mchezo huo wa Coast Union ni muhimu kwao kwa vile ndio utakaoamua mustakabari wa ubingwa wao.

Katibu mkuu wa Yanga Laurance Mwalusako alisema kuwa mashabiki wao wajitokeze kwa wingi ili kuwatia hamasa wachezaji wao na kuweza kutoka na pointi tatu muhimu katika mchezo huo.

Alisema pamoja na kwamba bado pointi moja watangaza ubingwa lakini malengo yao ni kuakikisha wanachukua pointi zote sita walizobakiza na kuchukua ubingwa kwa kishindo.

Mwalusako alisema mashabiki wao wanatakiwa kuja kwa wingi siku hiyo ili kushuhudia timu yao ikikabidhiwa ubingwa wa halali walioupata baada ya safari ya miezi 10 kutoka mwaka jana mwezi wa nane.

Hata hivyo uenda Yanga ikatawazwa mabingwa mapema kama Coast Union wataifunga Azam katika mchezo wao utakaochezwa kesho katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Katika hatua nyingine Uongozi wa Yanga umekabidhi cheti cha shukurani kuwa kuitumikia Yanga kwa miaka 11 mfululizo toka miaka ya 1960 aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo ambaye pia ni marehemu Athuman Kilambo kilichotokea Machi 10 mwaka huu.

Mwalusako alisema kuwa cheti hicho kimekwenda sambamba na rambi rambi ya shilingi 500,000 ambayo walitoa siku ya msiba.

Alisema klabu hiyo imeamua kuwatunza vyeti wachezaji wake wa zamani na kwamba wameanza kwa mchezaji huyo ambaye ni marehemu na wanaendelea kutoa vyeti hivyo kwa wachezaji wengine ambao wameitumikia Yanga kwa kipindi kirefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Waingereza wana msemo huu-"It ain't over till (or until) the Fat Lady sings" yangu macho

    David V

    ReplyDelete
  2. Ni Coastal Union na siyo Coast Union.

    Na hakika wagosi wa kaya wanaanza kurudisha viwango ya Coastal Union iliyowahi kuwa klabu bingwa ya Ligi Kuu Tanzania miaka ya nyuma.

    Mdau
    Coastal Union Fan

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...