Mwizi wa mkongo wa mawasiliano amekamatwa akiwa na vipande vya mkongo maeneo ya boko darajani jijini Dar es salaam. Matukio kama haya yamekuwa ni vipingamizi katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu.Kutokana na hali hiyo, sisi kama wadau wa mawasiliano, tunapenda kuwaasa Watanzania kwa ujumla, kama kweli tuna uzalendo wa kweli na mapenzi ya dhati na kampuni yetu ya mawasiliano inabidi  kujitoa zaidi katika kufanikisha usalama wa miundombinu ya kampuni yetu. Kwa matukio yeyote kama haya naomba msisite kutoa taarifa polisi au toa taarifa kwa namba zifuatazo:- 0737206622 , 07372066230737206624 ,07372066250737206626.

MSEMAJI
OFISI ZA MKONGO WA TAIFA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2013

    Nakumbuka Professa mbawalla alipokua Iringa ktk jitihada za kutandaza mawasiliano ya mkongo wa Taifa nilimsikia akisema kwa kuwaasa watanzania hasa wanaoishi maeneo ambayo nyaya za mkongo zitapita kua hizi nyaya si shaba, si dhahabu wala kopa hazina thamani yoyote hivyo kuwataka wasithubutu kukata na kwenda kuuza wakidhani zinathamani.Huyu jamaa kwanza kachoka kinoma, yaani anaonekana kama yu mgonjwa, anyway apewe adhabu ambayo itakua fundisho kwa wengine na siku ya kuhukumiwa wamtoe ktk vyombo vyote vya habari ili kufikisha ujumbe.Iwapo kweli tumedhamiria kukomesha uharibifu huu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2013

    Haki tena! hii yote ni umasikini wa roho na mwili!

    ReplyDelete
  3. Mbona hatoki midamu? sasa ndo nini kumwacha bila MANUNDU? HUYU alitakiwa amwagiwe mafuta ya taa then KIRIBITI kifanye kazi yake! pambaf

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2013

    Wala hakuna sababu ya kumgunga jela mwizi huyu. Apigwe bomba tuu arudishwe kwao Ethiopia. Hiyo ni adhabu tosha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2013

    huyu jamaa bado ana characteristics za kuishi porini na wanyama.adhabu yake itangazwe hadharani na bunge likae chapuchapu kukazia adhabu yake sioni adhabu inayomstahiri.jana nilishangaa kuona kuna mtu alitobolewa macho na polisi ndo nagundua kumbe inawezekana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2013

    yaani jamaa kachoka kweli; mimi naona apewe chakula ale; maana naamini njaa kali ndio iliyompeleka kuiba

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2013

    Mtizame hali yake,taaban
    Pengine anakufa na njaa,lakini sisi twataka akae kimya na njaa yake wakati sisi tulio na kila kitu twafaidi mitandao na muziki wetu wa kizazi kipya. Mpeni kazi na wizi wake muone utapotea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...