Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt. Kamugisha Kazaura ametoa mada kuhusu mkakati wa TTCL kusambaza mawasiliano ya kasi katika majengo nchini wakati wa mkutano wa bodi ya Usajili wa Makandarasi ( Contractors Registration Board (CRB) ambapo pia bodi hiyo ilikuwa ikiadhimisha miaka kumi na tano tangu kuanzishwa kwake.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na makandarasi takribani 800 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini, Dkt. Kazaura aliwaeleza nia ya TTCL kusambaza mawasiliano ya kazi katika majengo mbalimbali hapa nchini na kuomba ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa makandarasi kujenga majengo ambayo yatakuwa yamewezeshwa tayari kuunganishwa na huduma za mawasiliano ya kasi " Broadband Ready Buildings".
Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akiwasilisha mada kwenye mkutano huo, kushoto ni Eng. Samuel D. Shila kutoka kampuni ya Service Consult Ltd na kulia ni Bw. Mringi Kitaly kutoka Msafiri Infrastructure and Mining Solution.
baadhi ya washiriki wakifuatilia mada hiyo kwa umakini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akifafanua jambo kuhusu mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa waandishi wa habari na wateja waliotembelea katika banda la TTCL.
Dkt Kazaura (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa bi. Josephine Mwakapugi kuhusu huduma zitolewazo na TTCL.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2013

    TTCL endeleeni kuupiga usingizi mnono. Anzisheni huduma za simu za mkononi na nyie pamoja na kutoa huduma bora wateje watakuja wenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...