Mwandishi wa Clouds TV Austin Bayadi ( wakwanza kushoto) akibonyesha kitufe cha komputa wakati wa droo kubwa ya mwisho ya kumtafuta mshindi wa shilingi million 50 wa promosheni ya Amka millionea ambapo bwana Layakal Akbar Thawer mkazi wa Dar es salaam aliibuka mshindi wa promotion hiyo. Wakishuhudia ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando(aliyekaa katikati) akifatiwa na mwakilishi wa bodi ya michezo ya Bahati Nasibu Emmanuel Ndaki akifatiwa na Afisa masoko wa Airtel Khalila Mbowe.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando(katikati) na Afisa masoko wa Airtel Khalila Mbowe kwa pamoja wakionyesha droo ya kumtafuta mshindi wa millioni 50 wa Amka millionea inavyotafuta mshindi wakati wa droo hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Moroco na kushuhudiwa na Waandishi wa habari, akishuhudia kulia ni mwakilishi wa bodi ya michezo ya Bahati Nasibu Emmanuel Ndaki.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando(aliyekaa katikati) akiongea na wandishi wa habari (hapo pichani) wakati wa droo kubwa ya mwisho ya kumtafuta mshindi wa shilingi million 50 wa promosheni ya Amka millionea ambapo bwana Layakal Akbar Thawer mkazi wa Dar es salaam aliibuka mshindi wa promosheni hiyo. Kushoto ni mshindi wa million 15 wa promosheni ya Amka milionea bwana Juma Ibrahim Hiza mkazi wa Dar es Saalam na kulia ni mshindi mwingine wa shilingi milioni 15 Bwana Adnan Ayub Khan mfanyabiashara Simiyu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Amka millionea na kumzawadia mshindi wa droo hiyo kitita cha shilingi million 50.

Droo hiyo kubwa na ya mwisho ilifanyika katika makao makuu ya Airtel morocco na kushuhudia na waandishi wa habari ambapo mkazi wa Kariakoo Dar es Salaam Bwana Layakal Akbar Thawer mwenye umri wa 60 mafanyabiashara wa duka la rangi aliibuka kuwa mshindi wa millioni 50 na kutangazwa rasmi kuwa mshindi.

Akiongea wakati wa droo hiyo, Mkuu wa kitengo cha Masoko wa Airtel Levi Nyakundi alisema, Mpaka sasa Airtel kwa kupitia promosheni ya Amka millionea imewazawadia watanzania na wateja wengi nchini. leo tunashuhudia bwana Akbar akiibuka kuwa mshindi wa pesa taslimu shilingi million 50 kupitia promosheni hii ya Amka millionea na Airtel. Hii inathibitisha thamira yetu ya kutuoa huduma bora na bei nafuu huku tukiendelea kuwazawadia watanzania na wateja wetu kwa kupitia promosheni mbalimbali ikiwemo hii ya Amka millionea.

Tunaahiidi kuendelea kuboresha huduma zetu na kuhakikisha tunawafikia watanzania wengi zaidi, mpaka sasa kwa kupitia huduma ya Airtel yatosha wengi wamepata unafuu wa gharama za mawasiliano na kuwezeshwa kupiga simu kwenda mitandao yote nchini na kushuhudia kuwa kweli Airtel yatosha.

Tunaamini kwa kuendelea kuongeza ubunifu katika huduma zetu na kuwazawadia wateja wetu kwa kupitia promosheni mbalimbali pamoja na huduma bora zikiwemo za kibenki kupitia Airtel money na huduma ya internet ya kasi zaidi ya 3.75G wateja wataendelea kupata suluhusho la mawasiliano na za kimtandao zilizo bora , za uhakika na gharama nafuu aliongeza Nyakundi.

Akiongea kwa njia ya simu mshindi wa shilling million 50 bwana Layakal Akbar Thawer alisema “ mimi nimekuwa mteja wa Airtel kwa miaka 7 sasa na nafurahia huduma zao, napenda kuwambia watanzania washiriki promosheni hizi nao wananafasi ya kuibuka washindi.

Promosheni ya Amka milionea ilizinduliwa rasmi mwenzi December mwaka jana na kuongezewa muda wake mwenzi machi mwaka huu, mpaka sasa wateja zaidi ya1458 na pesa taslimu zenye thamani ya zaidi ya shilingi million 626 zimezawadiwa kwa washindi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.

Mshindi mwingine wa shilingi million 50 alipatikana na kuzawadia mwenzi watatu naye ni Mwalimu wa shule ya msingi na mkazi wa manyara kiteto bwana Grayson Safieli Kabora , huku washindi wa shilingi million 15 wakiwa ni pamoja na Juma Ibrahim Hamza umri wa miaka 30 na mkazi wa kawe Dar es Saalam na Adrian Ayub khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara Simiyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2013

    Safi AIRTEL ila niwashauri jambo moja.vocha zenu za sh 1000 zina viwango duni sana nikiwa Tz nimekula hasara sana ukizingatia ndo sie walalahoi tunakimbilia ukikwangua inaondoka na namba zote ukipika customer service wanakuweka siku nzima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...