
Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini, Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusheherekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi.
Siku ya July 6, 2013 hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo
207 w Hampton Pl,
Capitol Height, MD
Mambo mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, Mitindo ya mavazi kutoka Tanzania na hapa Marekani, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani na hapa Marekani yote ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili
TEGA SIKIO, HABARI ZAIDI ZITAFUATA
-------------------------------------------------------
kwa wajasiliamali ambao wangepenga kudhamini na kuijipatia meza ya kutangaza bidhaa au shughuli wazifanyazo tafadhali wasiliana 301 613 5165, 301 661 6696 na 301 792 8562 mwisho ni June 1, 2013 Asante
NO COVER CHARGE, FREE DINNER
''Haya wahudhuriaji ni wakati wa MAAKULI KAENI WANNE WANNE''
ReplyDeleteMjiandae ndoo za maji ya kunawa zinapitishwa muda si mrefu!
Huu ni utamaduni wetu waTanzania wa Takrima tofauti na jamii zingine za Jirani zetu ambapo ikifanyika sherehe ama unapookutana na mtu sehemu kwa Miadi ujiandae kwa kulipia kila kitu hadi Vinywaji na Chakula.
Kwa hivyo Waandaaji wa shughuli hii wamezingatia Utamaduni wetu Mzuri kwa kusema NO VOVER CHARGE, FREE DINNER!!!