Mahakama ya Rufaa imemrudishia Ubunge wa jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM Dkt Dalaly Peter Kafumu (pichani kushoto), baada ya kushinda rufaa aliyokata baada ya Mahakama Kuu kanda ya Tabora kumvua Ubunge kufuatia  madai ya kukiuka utaratibu wa uchaguzi wakati wa Kampeni katika Kesi iliyofunguliwa na Bw. Joseph Kashindye aliyekuwa Mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA.


Dkt Kafumu anakuwa mbunge wa pili wa CCM kurejeshwa mjengoni wiki, hii baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania, imethibitisha Mhe Aeshi Hilaly (pichani chini) kuwa mbunge halali wa Sumbawanga Mjini baada ya kushinda rufaa aliyokata kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, iliyomvua ubunge.

Hilaly alivuliwa ubunge na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Bethuel Mmila Aprili 30, 2012, kutokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kupitia CHADEMA,  Bw. Nobert Yamsebo. 

 Mhe Hilaly na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) walikata rufani kupinga hukumu hiyo na zote zilisikilizwa kwa pamoja na jopo la Majaji watatu, Edward Rutakangwa, Profesa Ibrahim Juma na Steven Bwana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...