Balozi wa Tanzania nchini Mozambique,Mhe. Balozi Shamim Nyanduga aliitisha kikao cha pamoja, kati yake na Viongozi Wastaafu wa Frelimo Jen.Alberto Chipande, Jen. Raymundo Pachinuapa na Viongozi wa Jumuiya za Watanzania , Mozambique Ubalozini Maputo,ili kuzungumzia mambo mbali mbali ya maendeleo.hilo ni tukio la kwanza kufanyika tangu Mhe. Balozi Shamim Nyanduga afike nchini Mozambique.
Mh. Balozi Shamimi Nyanduga (pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wastaafu wa Frelimo.Toka kushoto ni Col Lwimbo (DA),Jen. Pachinuapa na Jen. Chipande mara baada ya kikao hicho kumalizika.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mhe. Balozi Shamim Nyanduga (Hayumo pichani).
Kwawasio mfahamu Mzee Chipande, Mzee Chipande ni shujaa wa kweli yeye ndio alikuwa mtu wa kwanza kufyatua risasi na kumdondosha Mreno pamoja na Mbwa wake na hapo ndio kitimutimu kilipoanza kuikomboa Msumbiji toka mikononi mwa Wareno, na mpaka sasa Msumbiji ni huru ukiondolea mbali tafrani iliyojitokeza kati ya FRELIMO NA RENAMO.
ReplyDelete