Benki ya Dunia yatoa mikopo kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kuendeleza miji ujulikanao kama “Tanzania Strategic Cities Project” (TSCP) ambao umeundwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo kasi kubwa ya ongezeko la watu, miundombinu isiyokidhi mahitaji ya Miji husika na kutokuwa na rasilimali fedha kwa ajili ya kusimamia miundombinu na huduma nyingine za kijamii.
Mhandisi. Hanafy Mahmod (Meneja ushauri TSCP) akionyesha ramani yenye maeneo ya utekelezaji ya TSCP Dodoma kwa timu ya Benki ya Dunia na Ubalozi wa Denmark, pamoja na wawakilishi wa TSCP kutoka Mamlaka Saba ya Serikali za Mitaa na Mamlaka ya Maendeleo wakati wanatembelea maeneo husika, ambayo ilikuwa ni sehemu ya kongamano ya kutathmini shughuli za TSCP iliyofanyika Mei 27, 2013.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Mhe Aggrey Mwanri, (kati) akitoa maoni yake kuhusu ujenzi wa stendi ya mabasi Jamatini kwa timu ya Benki ya Dunia na Ubalozi wa Denmark, na wengine ni wawakilishi wa mradi wa uendelezaji miji Tanzania (TSCP) na wawakilishi kutoka serikali saba za Mitaa na mamlaka ya maendeleo wakati wanatembelea maeneo husika, ambayo ilikuwa ni sehemu ya kongamano ya kutathmini maendeleo ya TSCP iliyofanyika Mei, 2013.
Kaimu katibu mkuu, ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Jumanne Sagini(Kushoto) akikagua ujenzi wa daraja , eneo la Mwangaza –Kisasa mjini Dodoma. Wengine ni wawakilishi wa mradi wa uendelezaji miji Tanzania (TSCP).
Timu ya Benki ya Dunia na Ubalozi wa Denmark, wawakilishi wa mradi wa uendelezaji miji Tanzania (TSCP) pamoja na wawakilishi kutoka serikali saba za Mitaa na mamlaka ya maendeleo wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Mhe Aggrey Mwanri (hayupo pichani) wakati wa kongamano iliyofanyika Mei 2013 ikiwa ni sehemu ya kutathmini shughuli za TSCP katika Hoteli ya Dodoma – Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...