Katibu wa Naibu Spika na Mratibu wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Nd.Saidi Yakubu(kulia) katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Singapore Mhe.Goh Chong Tong(kushoto) wakati walipotembelea ofisi ya Jimbo lake kwa mafunzo ya vitendo kuona namna wananchi wanavyopata huduma toka kwa Mbunge wao.Wabunge wa Singapore hukutana na wananchi wao saa za jioni kwa kuwa ubunge ni kazi ya muda (part time) na wabunge wote huendelea na kazi/taaluma zao.Bunge la Singapore hukutana siku moja hadi tatu tu kwa mwezi na siku tano tu za ziada kwa mwaka ajili ya bajeti.Wengine pichani ni washiriki toka Afrika Kusini, New Zealand, Australia na Katibu Mkuu wa Chama cha Wabunge toka nchi za Jumuiya ya Madola, Dr William Shija.
 Mbunge wa Busanda, Mhe Lolesia Bukwimba akifuatilia mada wakati wa Semina ya 24 ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola inayofanyika nchini Singapore.Semina hiyo ina lengo la kuwaongezea wabunge na watumishi wao juu ya kazi zao ambapo mada mbali mbali zimekuwa zikitolewa ikiwemo majukumu ya mbunge kusimamia maadili ya kibunge; Uongozi wa Bunge na Huduma kwa Wabunge; Kanuni za Bunge na Umuhimu wa Kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni; Utungaji Sheria na Majukumu ya Jimbo na pia nafasi ya Teknohama katika kurahisisha kazi za Mbunge ikiwemo matumizi ya Mitandao ya kijamii
Washiriki wa Semina ya 24 ya CPA wakiwa katika picha ys pamoja ndani ya ukumbi unaotumiwa kwa elimu kwa Umma juu ya Bunge katika Bunge la Singapore. Picha kwa hisani ya Ofisi ya Bunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...