Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;
1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam.
2. KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu zilizotajwa hapo juu waweze kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.
Tume haitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hicho kwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam.
Angalizo:
Chuo cha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati husika tuu.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
Hawa jamaa wenye hiki chuo matapeli. Wameona Tanzania ni chi ya kuchezea .
ReplyDeleteNa sisi waTZ tumekuwa wa hivi hivi mno..Tuachane na rushawa. Watoto wetu watarithi nini? kama hata nchi jirani wametutambua kuwa rushwa tunaibembeleza.
TCU kwa nini mnaleta mkanganyiko ?
ReplyDeleteKwa nini mna complicate sana mambo?
Kutokana na kasi ya maendeleo inayokwenda sambamba na kasi ya kukua kwa Uchumi wetu na mahitaji ya Taaluma hamkustahili kukwamisha jitihada ongezeko la Taasisi zinazotoa Elimu za juu.
Kama vigezo ni upungufu wa Wakufunzi na Sifa za Taaluma kwa nini ninyi TCU msitoe usimamizi ama mchango wa kuwatafuta Wataalamu hao badala yake mnakwamisha utolewaji wa Elimu za juu?
Hebu angalieni Takwimu hizi juu ya Idadi ya Taasisi za Elimu ya juu zinazotoa Post Graduate, Masters na PhD. ktk nchi za wenzetu ukilinganisha na ukubwa wa Uchumi wao:
1.KENYA:
-Universities za kutoa PostGrad.MA na PhD. ni 20+
-Uchumi wao ni GDP US$ 35 Billion na kasi ya kuku GDP ni 4.5%
2.RWANDA:
-Universities za kutoa PostGrad.MA na PhD. ni 3+
-Uchumi wao GDP ni US$ 10 Billion na kasi ya kukua GDP ni 8.1%
3.ANGOLA:
-Universities za kutoa PostGrad.MA na PhD. ni 7+
-Uchumi wao ni GDP US$ 104 Billion na kasi ya kukua GDP ni 3.9%
4.GHANA:
-Universities za kutoa PostGrad.MA na PhD. ni 30+
-Uchumi wao ni GDP US$ 39 Billion na kasi ya kukua GDP ni 14.3%
5.NIGERIA:
-Universities za kutoa PostGrad.MA na PhD. ni 50+
-Uchumi wao ni GDP US$ 243 Billion na kasi ya kukua GDP ni 7.3%
-----------------------------------
TUZINGATIE YA KUWA MAHITAJI YA ELIMU YA TAALUMA YANAKWENDA NA (i) KASI YA KUKUA KWA UCHUMI, (ii)UKUBWA WA UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII HUSIKA.
-----------------------------------
Je sisi Tanzania wenye Vyuo Vikuu VIWILI vya Post Grad. MA, na PhD. na wenye GDP ya US$ 23 Billion na kasi ya kukua ya 6.1% tutaubebaji Uchumu wetu kwa kasi na kupata maendeleo endapo CTU inakwamisha jitihada hizo za Taaluma kuimarika kwa kupata Wasomi na viwango vinavyokubalika?
Hivi Tanzania si hao TCU wataifanya iwe ktk Karne ya 21 kama ipo ktk Karne ya 12?
Enheee TCU,
ReplyDeleteNi vipi kuhusu ule mchakato wa Uhakiki wa Shahada za Wahitimu ambao wengi tayari wapo ktk Utumishi ikiwemo Serikali na Mashirika ya Umma?
Nadhani mngeanzia huko kwanza kuwabana waliokwisha zikamata ambao wengi wamezitia kibindoni ktk mtindo wa Kimagumashi kabla hamjawabana wanaozitafuta hizo Shahada hivi sasa!!!
Ninyi TCU kupanda kwa ubora wa Elimu ya Juu hakutokani na kubana uzalishaji wa Wahitimu.
ReplyDeleteMnatakiwa mjenge mazingira ya kukuza uzalishaji wa Wahitimu wa Shahada za Juu badala ya kubana.
Ni kuwa mtazalisha tatizo kubwa sana ktk Uchumi liitwalo FISCAL DEFICIT kwa miaka ijayo, kwa kuwa Mahitaji ya nguvu kazi yaani LABOR DEMAND ktk Sekta za Uchumi, hasa PARASTALA SECTOR (inayohitaji Wafnyakazi WAZALENDO, huku PRIVATE SECTOR ikiwa inaweza kuajiri hata Wageni endapo Wazalendo wakikosekana) hayatawiana na upatikanaji wa Wanaokuwa na sifa husika.
Mngezingatia kwanza Labor Economics badala ya kuegemea zaidi kwenye Regulations, mlihitaji mjenge Mazingira ya kukuza na sio kubomoa ama kukwamisha!!!
Ohooo!,
ReplyDeleteAma kweli wengi tutaendelea kubeba Maboksi, Kuchoma Mahindi na Mihogo huku tukiwa hatujaelimika!
Yaani Tanzania nzima ya watu 45 Mil. Shahada za Juu kwa sasa zitakuwa zinatolewa na University mbili tu?
Pana Mwandishi mmoja Maarufu sana wa Makala za kwenye Magazeti ya Kiingereza (English Columnist) lakini akiwa hana Shahada wala Stahsahada alinieleza ya kuwa anapata wakati mgumu sana akifuatwa na Wasomi tena wenye hayo ma PhD. na Masters zao waklimtaka awasaidie kuandika vitu kama:
ReplyDelete1.Report Writing
2.Analysis
3.Field study
Tena kwenye maeneo ambayo hata yeye mwenyewe Columnist hanaujuzi nayo!,,,,hao ndio Ma Holder wa Bongo.
Vipi kuhusu zile PhD. za ku-kopi na ku-paste za Mabosi ambao wengi tayari wapo ktk Utumishi tena Sekta nyeti?
Ama kweli Elimu ya Bongo maana yake ni Kuvuka Vidato na kuhesabu miaka ya Masomo!
ReplyDeleteSi mnaona ndio yale yale Msomi ana Graduate lakini hata barua ya kuomba kazi hajui kuandika?
Nasikia ma-Prof chuo hakina, Director ana PhD halafu anataka atoe PhD kwa wengine kama ni kweli hii inasomekaje kitaaluma na kiutaratibu? Noma!
ReplyDelete