Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Manumba akizungumza na Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika mafunzo ya kufanya Operesheni za Pamoja kati ya SARPCCO na EAPCCO.Mafunzo hayo yanafanyika jijini DAR Es Salaam.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Manumba akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi mbalimbali za Afrika ambao wanashiriki mafunzo ya kufanya Operesheni za Pamoja kati ya SARPCCO na EAPCCO.Mafunzo hayo yanafanyika jijini DAR Es Salaam.

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi. 

Wakurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai kutoka nchi 25 barani Afrika wametakiwa kutumia vizuri mafunzo ya Operesheni za pamoja ili kuweza kukabiliana na uhalifu ikiwemo vitendo vya ugaidi na uhamiaji haramu vinavyojitokeza katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kwa kasi hivi sasa.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Manumba wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka Umoja wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) Pamoja na Umoja wa Wakuu wa Polisi Afrika Mashariki (EAPCCO) kuhusu kufanya operesheni za pamoja kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.

DCI Manumba amesema uhalifu unaofanyika hapa nchini na ukanda huu wa Afrika Mashariki ndio huo huo unaotokea katika nchi nyingine hivyo ushirikiano na kubadilishana taarifa kutasaidia kutambua na kuweka mikakati thabiti ya kuweza kudumisha amani na usalama katika bara la Afrika.

“Kwa mfano suala la Wahamiaji haramu hatuwezi kupambana nalo sisi wenyewe kwa kuwa wanatoka katika nchi nyingine na hapa wanapita tu kwenda katika nchini nyingine hivyo lazima tubadilishane taarifa na kuwa na mkakati wa pamoja wa kuwabaini wanaofanya vitendo hivyo” Alisema Manumba.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wa Kimataifa INTEPOL kanda ya Afrika Mashariki kutoka Nchini Kenya Bw.Rego Francis amesema Majeshi ya Polisi yana wajibu wa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili waweze kutoa taarifa za uhalifu mapema kwa vyombo vya usalama ili ziweze kufanyiwa kazi mapema kabla ya matukio kutokea.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Polisi wa Kimataifa (INTEPOL) Tanzania Kamishna Msaidizi wa Polisi Gustavus Babile amesema Mafunzo hayo ya siku mbili lengo lake ni kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu na kuweka mikakati ya kufanya operesheni zitakazoweza kuutokemeza uhalifu.

Babile alisema kupitia mafunzo hayo wataweza kuandaa Operesheni zenye mafanikio zitakazoweza kushirikisha nchi nyingi katika kukabiliana na Ugaidi, Madawa ya kulevya, wahamiaji haramu, wizi wa magari na uhalifu wa aina nyingine unaotokea hapa Afrika. Mafunzo hayo yanafanyika baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kumi na nane wa Wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika SARPCCO ambapo katika maazimio yaliyofikiwa ni pamoja na kufanya operesheni za pamoja baina ya SARPCCO na EAPCCO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2013

    Masikini Tanzania . Serikali inatoa mafunzo ya kukabiliana na wahalifu bila kujua kuwa inawafundisha waharifu hao hao. Ohoooooo! pole sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2013

    Masikini Tanzania . Serikali inatoa mafunzo ya kukabiliana na wahalifu bila kujua kuwa inawafundisha waharifu hao hao. Ohoooooo! pole sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...