Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (pichani) amechaguliwa kwenye mchakato wa kumtafuta “kinara wa Benki wa Afrika”  kwa mwaka 2013 unaoendeshwa na  African Banker Awards chini ya African  Development Bank Group.

 Kinara wa Benki wa mwaka ni tuzo inayotolewa kwa Viongozi (CEO`s) wa sekta ya benki na fedha barani Afrika ambao wamepata mafanikio makubwa kwenye mashirika yao hivyo kuleta maendeleo katika sekta fedha na uchumi katika nchi zao na Afrika nzima kwa ujumla.
African Banker Awards imechagua  vinara watano wa sekta ya fedha Afrika  kuingia katika mchakato huo ambapo mmoja wao ndiyo atakayejitwalia tuzo hiyo. Zaidi ya Dkt. Charles Kimei, wengine waliongia kwenye mchakato huo na nchi wanazotoka kwenye mabano ni  Segun Agbaje-GTB Bank(Nigeria), Aigboje Aig-Imoukhede-Access Bank(Nigeria), Andrew Allly-Africa Finance Corporation(Nigeria) na Jao Figuerdo- Unico Bank.
Dkt. Kimei ni mtanzania wa kwanza kuingizwa kwenye mchakato huu tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo zaidi ya miaka kumi iliyopita, na ni mtanzania pekee kwenye kinyang`anyiro hicho ambacho kimekuwa kikitawaliwa na mabenki kutoka nchini Nigeria na Afrika ya Kusini. Hii ni fahari kubwa kwa taifa letu kwani Dkt. Charles Kimei ni mtanzania anayeongoza benki kubwa ya Tanzania inayoendeshwa na watanzania wenyewe.
Dkt. Kimei, ambaye ni mchumi mwenye stashahada ya uzamivu, amefanya kazi katika sekta ya fedha kwa zaidi ya miaka 30 akitokea Benki Kuu ya Tanzania alikokuwa Mkurugenzi wa Sera na Utafiti  kabla ya kujiunga na Benki ya CRDB mwaka 1998 kama Mkurugenzi Mtendaji. Akiwa Benki ya CRDB ameingoza kutoka Benki iliyokuwa ikijiendesha kwa  hasara hadi kuwa Benki inayoongoza nchini.
Chini ya uongozi wa Dkt. Kimei, Benki ya CRDB imeweza kupata mafanikio makubwa  ikiwemo kutoka kutengeneza faida ya Shilingi billion 2 mwaka 1998 mpaka kufikia Shilingi billion 108 mwaka huu, kuongeza mtandao wake wa matawi kutoka matawi 16 hadi matawi 97 mwaka huu. Katika kipindi hiki  pia Benki ya CRDB imekuwa kinara wa kuleta bidhaa bunifu kwenye soko ikiwemo kadi zenye nembo za kimataifa za MasterCard na Visa, ATMs za kutolea na kuweka fedha, mashine maalum za kulipa kwa kutumia kadi (POS), Mikopo maalum ya Microfinance na Wajasiriamali pamoja na kushinda tuzo za kimataifa za Chapa Bora yaani SuperBrands kwa miaka minne mfululizo (2010-2013) na  tuzo ya benki bora itolewayo na  Euro-Money mwaka 2004.

Chini ya uongozi wa Dkt. Kimei, Benki ya CRDB imekuwa benki ya kwanza ya kizalendo  kuvuka mipaka na kufungua kampuni tanzu katika nchi jirani ya Burundi hivyo kufungua milango ya ukuaji wa mahusiano ya biashara kati ya nchi hizo mbili na ukanda mzima wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kuingia kwa Dkt.Kimei kwenye mchakato huu wa kupata kiongozi bora  wa Benki wa Afrika kunakuja muda mfupi tu baada ya kuteuliwa kwake bila kupingwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki nchini Tanzania (TBA). Mwenyekiti wa Chama Cha Mabenki huchaguliwa na benki zote wanachama wa TBA.
Tunamtakia kila kheri Dkt.Charles Kimei na Benki ya CRDB katika kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika tuzo hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2013

    Hongera, lakini wape somo wafanyakazi wako...wengine hawatoi huduma kama ipasavyo kama CRDB UDSM.Meneja kwa wateja haudumii ipasavyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2013

    Hongera Dr. Charles Kimei,

    Du kweli kazi umeifanya, yaani mpaka Watani zetu wa jadi Kenya hawamo ktk orodha?

    Kenya wana utitiri wa Mabenki lakini tatizo lao kubwa ni kuwa kweli huduma za Kibenki wanaziweza lakini ni vile wanajisifu sana wenyewe na sio kungoja kusifiwa.

    Kweli kutika kwa debe ndani mshindo mtupu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2013

    Kweli CRDB BANK PLC. Jembe la Chuma kama CCM!

    Ndio maana ni rangi ya Kijani rangi yao.

    Tena Makao Makuu ya African Development Bank yapo Nairobi-Kenya.

    Kenya na fujo zao na kelele za Mabenki yao hawamo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2013

    Tunakutakia kila la heri Dr Kimei. Unastahili kuzawadiwa kwa mageuzi ya kibenki ulioyafanya. Inabidi wafanyakazi wa chini yako waige hayo unayoyafanya ili kulinda hadhi ya CRDB. All the best. Ernest E.M.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 10, 2013

    aise meku hongera sana ni jambo la kijifunia makamanda mkionesha dira, tupo pamoja mpaka kieleweke

    peoples power !!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 10, 2013

    Charles Kimei,

    Kiukweli wewe ni mojawapo ya FAHARI KUBWA na HAZINA ya TAIFA,

    Sababu nyingine ya kujivunia kuwa Mtanzania,
    Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...