Wapo wale ambao wanadhani kuwa matajiri ndiyo watu pekee wanaostahili kusaidia wenzao katika jamii ambao kwa namna moja au nyingine wana shida au wapo katika mazingira magumu.
“Hiyo si kweli kwani kama wahenga walivyo sema na kuamini kuwa siku zote kutoa ni moyo na siyo utajiri,” amesema Lion Wilson Lion Ndesanjo, ambaye mwanzoni mwa mwezi huu alichaguliwa kuwa Gavana wa jimbo la 411B linalozijumuisha Tanzania na Uganda katika mkutano ulioyanyika Nairobi, Kenya.
Bwana Ndesanjo ni mfanyabiashara katika masuala ya bima na uendelezaji majengo. Vilevile ni mjumbe wa bodi katika taasisi mbalimbali.
Akiongelea mipango ya Club ya Lions hapa Tanzania, alisema kipaumbele kitaendelea kuwekwa katika kuwasaidia wasioona na wenye maradhi ya macho pamoja na wale ambao hawasikii.
Lions Club hali kadhalika itaendelea kutoa ufadhili wa matibabu ya maradhi ya moyo ndani na nje ya nchi, pamoja na wale wanaosumbuliwa na ugoinjwa wa kisukari.
Eneo jingine ambalo litalitiwa mkazo ni upatikanaji wa maji mijini na vijijini, pamoja na kuwasaidia walioathirika na pombe pamoja na madawa ya kulevya.
Club itaendeleza kampeni dhidi ya madawa ya kulevya ambapo vijana na watoto watalengwa katika kupewa elimu ya kujitambua na kutoa tamko la HAPANA kwa MADAWA ya KULEVYWA.
Gavana mpya wa Lions Club,Wilson Lion Ndesanjo akikabidhiwa Cheti mara baada ya kuteuliwa kuwa Gavana mpya wa jimbo la 411B linalozijumuisha Tanzania na Uganda katika mkutano ulioyanyika Nairobi, Kenya.
Gavana mpya wa Lions Club,Wilson Lion Ndesanjo akitoa hoyuba yake muda mfupi baada ya kuchaguliwa.
Akikabidhiwa Kikombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...