Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu Kasulu, mkoani kigoma Valerian Nickodemus Kamugisha akinyannyua kwa Furaha sehemu ya fedha Sh 100 Milioni alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom Mehala iliyomalizika hivi karibuni. Kamugisha amekabidhiwa fedha zake hizo leo jijini Dar es salaam na kuamua kuzifungulia akaunti katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela na Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa.
Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa akimtambulisha kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mshindi wa Promosheni kuu ya Mahela iliyomalizika hivi karibuni Valerian Nickodemus Kamugisha (kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi kitita chake cha zawadi ya sh. 100 Milioni iliyofanyika makao makuu ya NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.
Valerian Nickodemus Kamugisha (katikati) akipokea kitita cha sh. 100 Milioni kutoka kwa Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom MAHELA. Hafla ya makabidhiano imefanyika makao makuu ya benki ya NMB ambako mshindi huyo amechagua kufungua akaunti kuhifadhi fedha hizo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2013

    Duhhh!

    Valerian N. Kamugisha umefunika kinoooooma, ungewaambia Mabosi wa Vodacom na NMB wakuletee KITOROLI Kidogo kama cha Supamaketi cha kuubebea Mzigo wako kutoka hapo hadi Benki!

    Huoni ungali Kijana mdogo huku ukiwa na MIKONO midogo na michanga kabisa (isiyoweza kubeba Mibunda yote hiyo kwa mara moja) lakini Mwenyezi amekuona?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2013

    Kijana umetunukiwa viliyo!

    Kilichobaki usali sana kuomba upate mwongozo mwema.

    Kwa kuwa hapo tayari 'michupi' imekuona wataanza kukuwinda na kukutega ili mradi wakufilisi!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2013

    Kweli Mungu Mkubwa na pia Mwenyezi ni Tajiri saaaana!

    Hebua angalia bwana mdogo wapo watu wanatafuta fedha kwa bidii na kasi ya ajabu na ya kutisha!!!

    Wapo wanaotafuta kwa njia zotezote halali na haramu ili mradi wapate Fedha.

    Hayo dogo ni mafao yako ya Maisha ya kuteuliwa na mwenyewe SIR GOD, asiyekuwa na Mhsirika, majungu wala Fitina, yule ambaye akikuchagua, WATABEBA MAKARAI YA ZEGE LAKINI HAWATAWEZA KUZIBA!

    Lakini wewe mwanawane na zali lako, ile Taaap umenyanyuka na MIBUNDA!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2013

    Wauuuu !!!!!!!!

    Kudadadadadadeki si mtamtaka?

    Dogo ameyafunga maisha magumu Mabao 100 Million kwa Bila (100 Mil.-0)!

    Baada ya kukabidhiwa Bao la matokeo ya Mchezo wa Maisha linasoma:

    VALERIAN KAMUGISHA (Mabao)-100 Mil.
    MAISHA MAGUMU (Mabao)-0

    Hadi raha amechagua hadi shati la Rangi ya ''wekundu wa Mapesa'' (sio Simba wa Msimbazi waliofungwa 2-0) bali Minoti!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2013

    Ohooo unajua Dogo?

    Ukitoka hapo hiyo Kadi ya Benki mpelekee Bibi Mzaa baba au mama Kijijini akakufichie Darini !!!

    Halafu wewe kimya kimya urudi Chuoni kuendelea na Masomo.

    Kaa mguu pande mguu sawa kukwepa kuubeba MZIGO WA WACHUNAJI MIJIMAMA!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2013

    Fanya yoooote Kijana mdogo lakini nakushauri usisahau kufunga suruali yako ZIPU!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2013

    Hapo baada ya kupokea mzigo wako huku watu wakifahamu tukio hilo ndio utawatambua maadui, wanafiki na marafiki wa kweli!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2013

    Ukiwa Msituni jihadhari sana na wanayama wakali.

    Lakini ukiwa Mijini jihadhari na michupizzz (hawa kitengo sana,Mafia, Majambazi sana wanatisha, wanawapenda watu wakiwa nazo tu) usije ukafa ukiwa ungali kijana na mahela yako mkononi!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2013

    Dogooooo kimbia weeeee, kimbia upesi wanawake hao wanakukimbiza nyuma yakooo!!!

    Ogopa sana wasije wakakufilisi haooooo!!!

    Wahi haraka Benki ukitoka kuziweka jikaushe kabisa kama hunazo urudi ukasome Chuoniii!

    Ukitulia mtafute wa ukweli umuoeee!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 27, 2013

    Hii aibu sasa, mahela utafikiri tupo Zimbabwe. Tufikirie kuanzisha malipo mbadala e.g Cheque or credit cards kubeba manoti namna hii si salama.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 27, 2013

    Yote tisa Kijana kumi ogopa kupakatwa!!!

    Utabembelezwa hadi ujisahau, lakini zingatia kushikilia furushi la MAPESA yako sawa wasa.

    Utashikwa hadi Masomo ya Ualimu utayaona kama ni ya Udakitari, kisa nini? umekamata Mihela!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 27, 2013

    Eti "masomo ya ualimu utaona kama ya udakitari "

    Tungo tata, kwa maana ni marahisi sana ama ni masomo yasiyo na maana?

    Kwa vyovyote vile ualimu ni fani nzuri basi tu wabongo hatujalijua hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...