Hili ni dampo la taka ngumu ambalo naamini kabisa kuwa si rasmi kuwepo katika eneo hili la makutani ya Barabara ya Mwai Kibaki (zamani Old Bagamoyo rd) na Kisiwani pembeni tu ya Jengo la Shoppers Plaza ambali kiukweli kabisa,linatia kinyaa kuliona hasa katika eneo hili la wazi namna hii.hapo awali Dampo hili lilioanza kimasihara masihara tu,lakini kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga nalo limekuwa likiongezeka.na linaonekana kufumbiwa macho kabisa na wahusika ambao ndio wenye jukumu kubwa la kuhakikisha maeneo mbali mbali ya jiji yanakuwa safi.sasa sijui wanafanya makusudi,uzembe au ndio hawana muda wa kuingia huku mitaani kushughulikia haya??
Cheki mauchafu yalivyorundikana....!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2013

    huku mtaani kila kitu ni dili tu. kampuni za kuzolea taka ni dili za madiwani na watendaji kwahio hapo usikute mkandarasi hakulipwa kwakuwa hakutoa chochote kwa waheshimiwa. watendaji kata wa mijini na wao wao ni full biashara tu, ishu lazima iwe na maslahi kwake ndio itafanyiwa kazi.

    ReplyDelete
  2. Kwa kuwa hawa jamaa wa sumatra wanasimamia usafiri jijini wafanye na wa usafi pia ilikwa faini zao watu wangekoma wallah!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2013

    manispaa ndio wahusika wanaostahili kusimamia usafi wa jiji

    meggie impostra

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2013

    Kwa kweli uchafu umekithiri hivi sasa hata hizi barabara za mwendo kasi zinazoendelea kujengwa wanaweka taka bila aibu yaani malundo na malundo kuanzia magomeni hadi ubungo. Watanzania tunatakiwa kubadilika. Ustaarabu hauna darasa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2013

    hatuna pesa ya kazi hiyo, bajeti yake bado kusomwa bungeni, ikisomwa tu tutazoa kwa kasi inyostahili kufuatana na kasi ya bajeti (ukubwa wa mshiko unaomegeka)!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2013

    Mie nadhani kunahaja ya kuunda taasisi ambayo itasimamia kazi hiyo tu, kwakuwa halmashauri zimeonekana kutokuwa makini na kero hii kwa muda mrefu sana na badala yake inafanywa kwa rushwa tu jambo ambalo linafanya majiji yetu kuwa machafu hususani DSM. Mitalo haizibuliwi, wananchi hawahamasishwi na kupatiwa elimu sahihi kuhusu usafi wa jiji.Hapa tupate taasisi itakayo jiendesha kwa faini kwa wachafuzi na ruzuku kidogo ya serikali.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2013

    Wewe unasikitisha kwani haujui kweli kwamba halmashauri ya jiji ndio inasimamia na inayotakiwa kuhakikisha mazingira ya jiji yanaenda vizuri na mji ni msafi?

    Kama waki outsource kazi za usafi kote jijini au katika maeneo bado lazima wao ndio wakufuatilia kuwa kazi inafanyika.

    Please acha siasa/kujigonga/kuogopa toa ujumbe uwafikie directly na kutochukua short cuts eti unatuuliza hapo unaonyesha nini?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2013

    unajua sasa viongozi hao hao ndo wafanyabiashara..hile kampuni ya Green vipi tena kwishakazi au?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...