Mdau Innocent Melleck na mai Waifu wake Hanifa Hussein wakikata ndafu wakati wa tafrija ya ndoa yao iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Sunset (Tembo Hall),Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Maharushi Innochent Melleck na mkewe Hanifa Hussein wakiwa sambamba na wapambe wao kwenye tafrija hiyo ya ndoa yao iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Sunset (Tembo Hall),Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Maharushi wakiwa ni wenye nyuso za furaha na bashasha tele.
Bwana Hasuri Innocent Melleck
Bi. Harusi Hanifa Hussein.
Hongera Binti Hussein, lakini je mmeoana kwa dini gani?
ReplyDeleteMdau hapo juu,ndio wale waleeee!!!!ndoa ni makubaliano ya watu wawili ambapo wao wenyewe kwa mapenzi yao wameamua kuishi pamoja kama mke na mume,wewe inakuhusu nini,subiri wanao watakapotaka kuoa au kuolewa ndio uje na maswali yako.
ReplyDeleteMdau wa Kwanza hiyo ni moja kwa moja Ngoma kwa DC aka Mkuu wa Wilaya!!!
ReplyDeleteMdau wa kwanza uko sawa. Ni lazima uulize dini kwanza. Maana katika uislamu hakuna ndoa kati ya muislamu na mkristo. Hakuna.
ReplyDeleteMdau wa kwanza unamuharisho wa mdomo, mdau wa pili umelonga vizuri sana, asubiri wanae wakue (kama anao), watamletea siyo dini tofauti tu, na taifa tofauti,mahaba mahabuba yana hatari na hayana upeo, macho yakiona moyo ukapenda basi hapo mambo mswano, hakuna cha dini wala mjomba wake dini gani.Wamehusudiana wewe watakie kheri usepe kivyako.
ReplyDeleteMdau wa kwanza unamuharisho wa mdomo, mdau wa pili umelonga vizuri sana, asubiri wanae wakue (kama anao), watamletea siyo dini tofauti tu, na taifa tofauti,mahaba mahabuba yana hatari na hayana upeo, macho yakiona moyo ukapenda basi hapo mambo mswano, hakuna cha dini wala mjomba wake dini gani.Wamehusudiana wewe watakie kheri usepe kivyako.
ReplyDeleteMdau wa kwanza....inaelekea bint Hanifa na Innocent wana madhehebu tofauti, na wamependana na wakakubaliana wakaoane kwa DC. sasa wewe inakuuma nini? mbona watu hawakukemea Dodi alivyokuwa na mahusiano na Diana? au Arafat kuwa na mke mkatoliki? vipi wewee? Au WATU kama Inno hawaruhusiwi kuoa AINA ya akina Hanifa? na badala yake ni unataka kuhalalisha KAKA zake Hanifa kuwaoa DADA zake Inno? je umeelewa hii?
ReplyDeletemwanamke muislam ndio tatizo sio mwanamme muislam. wewe uliza tu utapata jibu lakini hapo ndoa ya kiserikali tu mungu haijui hiyo ndoa utake usitake labda ubishe tu. ushafahamu wewe mtu wa maisha wa miaka 60 sisi tunatazama maisha milele.
ReplyDelete