Na Woinde Shizza,Arusha
BENDI ya Jahazi morden taarabu chini ya muimbaji mashuhuri Mzee Yusuph inatarajia kunogesha usiku wa kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Arusha
(Redd's Miss Arusha 2013) itakayofanyika June 08 mwaka huu katika
ukumbi wa triple A jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa shindano hilo,Phidesia
Mwakatalima alisema kuwa shindano hilo litafanyika usiku wa jumamosi
june 08 katika ukumbi wa Triple A.
Alisema kuwa jumla ya walibwende kumi na tano 15 kutoka katika
vitongoji vitatu vya jiji la Arusha,watapanda jukwaani kuchuana vikali ili kuwezesha kupatikana kwa Redd's Miss Arusha 2013,vitongoji hivyo ni pamoja na
kitongoji cha Njiro,Arusha mjini (Arusha city centre) pamoja na kitongoji
cha Monduli.
Alibainisha kuwa mpaka sasa warembo wameshaingia kambini na tayari wameanza
kujifua kwa ajili ya shindano hilo huku akibainisha kuwa kwa mwaka huu
lazima mrembo wa Tanzania (Redd's Miss Tanzania) atokee mkoa wa Arusha
Alisema kuwa zawadi mbalimbali zitatolewa ikiwemo kuwasomesha warembo
katika vyuo mbalimbali lugha ya kiswahili ,kingereza pamoja na
kifaransa.
Shindano hilo lidhaminiwa na perfect choice super markety,libeneke la kaskazini
blog,trile A fm,Radio 5 fm,sunrise Fm,Mambo Jambo Fm,Aliance
francee,Geo Securty,Cassaranda wear,Meru Spring Water Pamoja na Otakef
Motel.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...