Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekemea vikali vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. 
 Akizungumza katika eneo la Kizota mkoani Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali. 
 Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote.
“Hivi watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali Rais Kikwete.
 Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo.
“Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.” Alisema kwa msisitizo
Taswira za uharibifu uliotokea katika vurugu hizo za Mtwara



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2013

    Ni sawa,

    -Almasi
    -Dhahabu
    -Madini
    -Kahawa
    -Maliasili

    Vimekuwa miaka nenda miaka rudi vikipatikana maeneo mengine nchini huku watu wa nchi nzima wakinufaika.

    Iweje leo watu wa Mtwara watake manufaa ya Gesi yawe kwao tu?

    Tunachotaka ni kuwa na uwazi ktk masuala haya ili tujue ni jinsi gani wwengi wananufaika na kutoa lawama na migogoro.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2013

    Hivi wana Mtwara mnafikiri Gesi imepatikana kwa bei ya bure?

    Mnaposikia Rasilimali yeyote ktk Uchimbaji au Uzalishaji wa Kiwango cha ukubwa wa juu utafutaji wake umegharimu Mamilioni ya Dollars !

    -MINERAL EXPLORATION
    -PRODUCTION
    -DEVELOPMENT

    Sasa hapo ktk E&P (Exploration & Production)ni hatua mbili tofauti ambapo Exploration ni utafutaji ambao ni GHALI SANA kitu ambacho Mtwara pekee isingeweza kuigharimia bila kutumia Rasilimali za Mikoa mingine kwa GHARAMA HIZO KUBWA SANA.

    Hivyo kama Raisi JK alivyosema, Rasilimali ni kitu cha wote kwa kuwa utaftaji wake hutumia GHARAMA zinazolipwa na nchi nzima kwa kiigharimu nchi na si Mkoa peke yake kama mnavyofikiri.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2013

    Hivi wana Mtwara mnafikiri Gesi imepatikana kwa bei ya bure?

    Mnaposikia Rasilimali yeyote ktk Uchimbaji au Uzalishaji wa Kiwango cha ukubwa wa juu utafutaji wake umegharimu Mamilioni ya Dollars !

    -MINERAL EXPLORATION
    -PRODUCTION
    -DEVELOPMENT

    Sasa hapo ktk E&P (Exploration & Production)ni hatua mbili tofauti ambapo Exploration ni utafutaji ambao ni GHALI SANA kitu ambacho Mtwara pekee isingeweza kuigharimia bila kutumia Rasilimali za Mikoa mingine kwa GHARAMA HIZO KUBWA SANA.

    Hivyo kama Raisi JK alivyosema, Rasilimali ni kitu cha wote kwa kuwa utaftaji wake hutumia GHARAMA zinazolipwa na nchi nzima kwa kiigharimu nchi na si Mkoa peke yake kama mnavyofikiri.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2013

    Ninyi WAMAKONDE huko MTWARA mkidai kuwa GESI ni mali yenu,

    Mbona gharama za kuitafuta Gesi Mtawara zimelipwa na Watanzania wote hapa nchini leo kweli ni haki mkidai peke yenu manufaa ya rasilimali?

    Je WASUKUMA wa SHINYANGA na MWANZA ambao tumekuwa tukitumia mauzo ya ALMASI, NG'OMBE na DHAHABU zao tokea Uhuru 1961 mbona hawaja lalamika kudai kunufaika na hizo mali zao peke yao?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2013

    Kitu kimoja ambacho serikali za nchi za Afrika zinatakiwa kujifunza ni kuhakikisha jamii inanufaika na rasilimaili zilizopo katika mazingira yao. Hii ndiyo njia pekee ya kuwafanya watu wajikie wanamiliki vitega uchumi vya nchi. Kitu kingine cha kuzingatia, vijana wasipokuwa na ajira ni kama bomu; tarajia mlipuko muda wowote. Yaliyotokea, Liberia, Sierra Leon na nchi nyingine kinaweza kutokea hapa kwetu kama viongozi wetu wataendelea kujali matumbo yao na kusahau maslahi ya wananchi wanaozidi kudidimia kwenye dimbwi la umaskini. Kuna siku watasema inatosha na ndio hapo neno AMANI litasahaulika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...