KAMISHNA Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akikagua Guard ya heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake kabla ya kuanza zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Magereza toka Mikoa ya Kanda ya Ziwa leo tarehe 4 Mei, 2013 katika viwanja vya Gereza Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Magereza akimvalisha Nishani ya Utumishi wa muda Mrefu na Tabia njema Mkuu wa Magereza Mkoa Shinyanga, ACP Abdul Kasim Mgwanda. Jumla ya Maafisa na Askari 42 kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wamevalishwa Nishani mbalimbali Leo tarehe 4 Mei, 2013.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja, akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Ally Nasoro Lufunga( wa kwanza Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anna Rose Nyamubi( wa pili kutoka kulia) Mara Baada ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa Leo tarehe 4 Mei, 2013.
Guard Maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja hayupo kwenye picha kabla ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza lililofanyika katika viwanja vya Gereza Shinyanga Leo tarehe 4 Mei, 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...