Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alianza ziara yake Same kwa kufika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mwalimu Herman Kapufi kujitambulisha.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi na ujumbe wake wakipitia baadhi ya kurasa katika kitabu hicho.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa(aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi (suti nyeusi) eneo lenye mgogoro wa mpaka katika Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamambaa; Kaimu Mkurugenzi wa Mipango wa TANAPA Dk. Ezekiel Dembe na Mkurugenzi wa Utumishi Wizara ya Maliasili na Utalii Said Msambachi.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa akitoa Taarifa ya Hifadhi ya Mkomazi kwa Katibu Mkuu Maliasili na Utalii pamoja na ujumbe wake.
Watumishi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi wakiwa makini kumsikiliza Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alipowatembelea.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi (wa pili kulia) akizungumza na watumishi wa Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamamba, Mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi Donat Mnyagatwa na Mkurugenzi wa Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Said Msambachi.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi katika picha ya pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akiangalia mbwa mwitu waliohifadhiwa katika uzio maalum kwa ajili ya kuwalinda Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.Picha zote na mdau Pascal Shelutete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2013

    ni vizuri kama haipo kwenye mitaala ya shule za primary mpaka sekondari kuwekwa masuala ya hifadhi ya mazingira pamoja na hifadhi za taifa, kupiga vita mambo ya uwindaji wowote wa leseni, uwindaji uruhusiwe kwa wanavijiji ambao wanakaa maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kitoweo na sio biashara. Nafikiri ni muhimu kuongezwa kwa topiki inayozungumzia utalii kwa ujumla. Na hata kama hatuna watalii kulinda mali asili zetu iwe kipaumbele ili vizazi vijavyo wasije kuona akina simba , chui nk katika picha tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2013

    Hivi mbwa mwitu wanalindwa kwani wana matatizo gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...