Na Abdulaziz Video
Imebainishwa kuwa Muamko mdogo wa elimu miongoni mwa jamii Wilayani
Ruangwa kunachangiwa na jamii wakiwemo Wazazi kutopenda kuchangia
elimu ya watoto wao ikiwemo Ufuatiliaji wa nidhamu na maendeleo ya
watoto wao.
Akifungua kikao cha wadau wa Elimu wilayani humo,Mkuu wa wilaya ya
Ruangwa,Bi Agness Hokororo alibainisha kuwa wilaya hiyo imejipanga
kuhamasisha jamii kushiriki katika kuboresha elimu huku serikali
ikijipanga kutoa motisha kwa walimu, mafunzo kazini pamoja na kutoa
motisha kwa walimu wapya.
Wilaya ya Ruangwa ina jumla ya shule 81 za msingi na 15 za sekondari
ambapo kuna walimu 488 kati ya 673 wanaohitajika huku Shule za
sekondari zina walimu 121 kati ya 256 na kati ya hao ni walimu 20 tu
wa masomo ya sayansi na hisabati
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Agness Hokororo akifungua kikao cha wadau wa Elimu wilayani Humo kinachoendelea katika ukumbi wa Yongolo,Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Ruangwa,Clemence Mwakasendo na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bw Issa Njinjo
Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika kikao cha wadau wa ELIMU
Wadau wa Elimu wilayani Ruangwa wakiwemo Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa
Wadau wa elimu wakifuatilia kikao kwa makini
Kikao kikiendelea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...