Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Mh. Abdalah Ulega akizungumza na wadau waliokutana leo kwa ajili ya kujadili Amani na Maendeleo ya Wilaya hiyo kufuatia machafuko yanayoendelea hivi sasa mikoa ya Kusini kutokana na Kutokuwepo Ushirikishwaji baina ya watendaji wa Serikali na Jamii hali inayochangia jamii nyingi Nchini Kukosa Imani na Serikali yao.
Baadhi ya Wadau waliohudhulia mkutano huo.
Na Abdulaziz video-kilwa
Serikali wilayani Kilwa imetakiwa kuwa na uwazi katika fursa
mbalimbali za maendeleo kwa kushirikisha jamii ili kufanikisha wilaya
hiyo kuinuka kiuchumi kupitia Raslimali zilizopo Wilayani humo.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wadau waliokutana leo kwa ajili ya
kujadili Amani na Maendeleo ya Wilaya hiyo kufuatia machafuko
yanayoendelea hivi sasa mikoa ya Kusini kutokana na Kutokuwepo
Ushirikishwaji baina ya watendaji wa Serikali na Jamii hali
inayochangia jamii nyingi Nchini Kukosa Imani na Serikali yao.
Wakichangia katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa PEC
wilayani humo na kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa
dini, siasa ,asasi za jamii na watendaji wa serikali waliokutana
katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa wilaya hiyo,Abdalah Ulega
kimelenga kuzungumzia hali ya amani ,usalama na maendeleo ya kilwa
ambapo alitoa fursa kwa wananchi hao kujadili kwa undani na kuweka
mikakati ya kuhakikisha Amani Inadumishwa ndani ya wilaya hiyo na
Mkoa.
Awali akitoa taarifa ya Mapato ya mrahaba wa Gesi asilia ya Songo
Songo kwa Wilaya,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Addoh
Mapunda alibainisha kuwa licha ya wananchi wanaoishi eneo la
Songosongo kunufaika na gesi inayopatikana kwenye kijiji cha
Songosongo alieleza Kuwa Madiwani wa Halmashauri hiyo wamepitisha 35%
ya malipo ya mrahaba huo wa gesi utumike katika kuboresha elimu
Nae Mkuu wa Wilaya Hiyo,Abdallah Ulega aliwasihi wananchi wa Wilaya
hiyo kujipanga na Kushirikiana na Serikali yao kudumisha Amani ikiwa
pamoja na kufungua fursa kwa Wananchi kueleza changamoto na kero
mbalimbali walizonazo kabla hawaichukia Serikali kutokana na Ushawishi
wa Dini na Siasa ikiwemo na Mataifa mbalimbali.
Kufuatia uwepo wa Gesi asilia ya Songosongo wilaya ya Kilwa upata
mrahaba wa Mil 100 kwa Mwezi ambapo asilimia 35 hutumika katika
kuboresha Elimu,Asilimia 20 kijiji cha Songosongo huku 45%
zikichangia katika shughuli za maendeleo wilayani humo.
basi jengeni chuo kikuu hapo; mbona munaleta mchezo. elimu ni mama wa kila kitu
ReplyDelete