KUNA ASKARI POLISI MMOJA PALE FERRY, DAR ES SALAAM,  JINA SIMFAHAMU ILA NI MWEUSI, PANDE LA BABA NA ANAPENDA KUVAA MIWANI MIEUSI WAKATI MWINGINE HUWA ANAKUWA NA KIPAZA SAUTI KUTUTANGAZIA ABIRIA TUNAOVUKA KWA KUTUMIA VIVUKO VYA KWENDA KIGAMBONI KUWA TUJIHADHARI NA WEZI PIA TUWE MAKINI TUNAPOINGIA KWENYE KIVUKO KUWA TUSIPITE PEMBENI KUNA UTELEZI. 
 YAANI ASKARI HUYU NI HODARI SANA KWA KAZI YAKE, SASA KWA HUU UTARATIBU ULIOANZA WA UKATAJI UPYA WA TIKETI ULIKUWA UNAJAZA MSONGAMANO WA WATU SANA WAKATI WA KUINGIA LAKINI NIMEPITA HAPO NIKAKUTA HUYU ASKARI AMEDHIBITI HIYO HALI YA MSONGAMANO NA WATU TUNASIMAMA MSTARI MMOJA NA KUKATA TIKETI YA KUINGILIA KWENYE KIVUKO KWA USTAARABU MKUBWA SANA BILA HATA YA KUSUKUMANA NA KURAHISISHA KAZI YA WAFANYAKAZI WA HAPO. 
KWA KWELI ASKARI HUYU NI MFANO MKUBWA WA KUIGWA. KAMA KWENYE FOLENI PIA YA MAGARI YANAYOSUBIRI KUINGIA KWENYE KIVUKO KUNGEKUWA NA ASKARI KAMA HUYU NAFIKIRI WALE WENYE TABIA YA KUCHOMEKA INGEKOMA KWA MAANA HAO WACHOMEKEAJI WANASABABISHA FOLENI.

WADAU KIGAMBONI
Askari mtajwa huyo anaitwa Koplo Francis  Zambi na pichani anaonekana akiwa kazini katika taswira hizi exclusive za Globu ya Jamii zilizopigwa baada ya wadau kuomba aonekane na ikiwezekana apandishwe cheo. Pamoja na kuongoza wapandao Ferry 'Komandoo' huyu pia ni mwanamaji na mpiga mbizi hodari wa kikosi cha Marine Police.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2013

    Kweli hata mimi juzi nimemkuta jioni akitupanga mstari mmoja, hivi kweli hawa viongozi wa kivuko hawawezi kumuweka askari mwengine pindi huyu anapokuwa hayupo? ni kero kero kero kwa kwenda mbele, hebu jalini watu kwanza pangeni watu wa zamu kuweka utaratibu wa kukata ticket maeneo yote ni fujo fujo fujo !

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2013

    Kuna watu wana uwezo wa kazi fulani kama huyu ni askari wa kweli, akipandishwa cheo na kupelekwa ofisini anaweza asifae tena kwa kazi hii. Huyu anatakiwa aongezewe mshahara kama motisha ili aendelee kufanya kazi hii kwa juhudi zaidi. Siku hizi malipo yanakwenda kulingana na kazi iliyofanyika sio vyeti!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2013

    safi sana,kwa kweli tunatakiwa tufanye kazi ili wale tunawatumikia waone na wakiri,kama hivi.Huyu jamaa apewe cheo na ikiwezekana double promotion na mkuu aandae hafla ambayo wadau tutahudhuria,inaongeza tija sana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2013

    Big up commandoo..hii nchi inahitaji watu kama hawa ndo itaendelea...huyu hata akinipiga mzinga nitamuelewa maana kazi yake anaifanya kwa ufasaha pia ..sio unakuta mi traffic yenyewe imekazana na rushwa tu...daladala zinavunja sheria yenyewe inaangalia tu...Apandishwe cheo hii hata ulaya ipo comments za watu zinapandisha mtu cheo...Kula tano askari!!
    mdau wa London.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2013

    Aisee mimi binafsi huyu askari namkubali sana,Mungu azidi kumbariki katika kazi yake,ikiwezekana awe rewarded kwa kazi hii kwa mchango wake katika jamii.kwa kuwa anajituma,yuko dedicated na anapenda kazi yake.Ahsanteni.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2013

    He looks serious for his job

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 30, 2013

    Huyu jamaa namkubari sana,siku moja nilivuka pale akaniambia nishushe abiria wangu na mie nisifunge mkanda na vioo nishushe na akanielewesha sababu za kwa nini nifanye yote hayo ,tena kwa utulivu hatua kwa hatua na vichekesho kadhaa,nikamwelewa kabisa hafu nikampenda ,ingwawa mwanzo niliona kama usumbufu vile na sikujua maana halisi ya maagizo yote yale.Hakutumia miamuri amri na matusi matusi kama wengi wao walivyozoea,ombi langu kwa mabosi wake,apangiwe kusimamia msululu wa magari utokao magogoni kuja feri,maana pale kuna ujanja wa watu kuchomekea msululu,inachelewesha sana kwa wanaofata utaratibu.Siku moja nilikaa kwenye msululu tangia saa a 12 jioni nikavuka saa 3 usiku,kisa wachomekaji

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2013

    Loo,mnamkumbuka yule askari alikuwa anaitwa 'SHARP'huyu naye anafanana na yule,sijui yuko wapi au ndo kesha sahaurika,wenye data mtujuze

    ReplyDelete
  9. IKIWEZEKANA APANDISHWE CHEO KUTOKA KOPLO HADI NYOTA MOJA, ILI AWEZE KUWASIMAMIA VIZURI ASKARI WENZAKE AMBAO HAWAJITUMI KAMA YEYE NA ASITOLEWE HAPO FERRY MPAKA DARAJA LIMALIZIKE KWA KUWA DARAJA LIKIMALIZIKA MSONGAMANO WA WATU UTAPUNGUA. KWA KWELI NAMPA BIG UP SANA KOPLO ZAMBI NAOMBA WAKUBWA WA POLISI WAMUANGALIE ZAMBI NI MFANO MZURI NA TASWIRA IMARA YA JESHI LETU LA POLISI.
    MDAU,KIGAMBONI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 30, 2013

    Hivi karibuni nilipotembelea nyumbani Tz nilibahatika kuvuka kwa kutumia kivuko cha Kigamboni ambapo nilimshuhudia askari huyu akiwa kazini. Lazima nikiri wazi kuwa nilivutiwa na ushupavu na kujituma kwake, sikujua kama kuna wanaotambua mchango wake hapo ferry. Tafadhari kama kuna mtu au yeye mwenyewe anaweza kunitumia namba yake ya simu kupitia blog hii nahitaji kumpongeza kwa juhudi zake

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 30, 2013

    Kijana huyu apandishwe cheo kwa kazi yake nzuri ya kuhudumia raia wa Tanzania.Ni kijana hodari naye apongezwe maana anaipenda kazi yake.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 30, 2013

    Dah huyu askar ni hodar aisee mara nyingine huwa anakuwa kurasini kunapokuwa na msongamano wa malori kuelekea gate namba tano hapo pia huwanyoosha madereva.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 30, 2013

    MIMI PIA NI MKAZI WA KIGAMBONI NA HUWA NINAMSHUHUDIA HUYU KAMANDA, PIA ANA MWILI WA KIASKARI NA HUWA ANAJITUMA NA HE IS VERY SERIOUS WITH HIS JOB WOTE WANGEKUWA KAMA YEYE BASI MAMBO YANGEKUWA MAZURI SANA KATIKA IDARA HII YA USALAMA WA RAIA.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 30, 2013

    nilisikiaga sharp alikufa sijui kweli? alikuwa kama huyu huyu,ila huyu jipande la baba.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 30, 2013

    Inasisimuwa kweli kweli.
    Big up kwa aliyepiga picha hizi na kuziweka hapa kwa taswira nzuri na za kusisimuwa.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 30, 2013

    Kwa utendaji wake mzuri wa kazi apewe ulaji kwa kuhamishiwa idara ya usalama barabarani (Trafiki)

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 30, 2013

    Hii safi sana,Nampongeza sana.

    Kama mabosi wake watatambua juhudi zake basi mtujuze pia.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 30, 2013

    Ahamishiwe TRAFFIC ndio kupandishwa cheo!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 30, 2013

    Huyu anastahili aongezewe mshahara mara dufu,ili iwe motisha kwake na wengine wamuige, anafaa sana; ni komandoo kweli kweli; i have seen the guy several times; ingawaje ukimfanyia mzaha anaweza hata kukurusha kichurachura

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 30, 2013

    very good,,!but he surpose to wear bulletproof for more self prevention

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 30, 2013

    Huyu ni askari wa kweli maana hana kitambi kama wale wengine huyu misukosuko yote anaweza kuikabili big up

    Chonde chonde usitoke kitambi kama wale mafisadu

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 30, 2013

    Nadhani sijavuka Kigamboni kwa kipindi kirefu sana lakini nimefurahishwa sana na kuona wapo watu wanawafurahia watenda mema bila kutaka rushwa. Asanteni kuifariji roho yangu. Swali michuzi utakuwa tayari kutupigia picha za askari tunaowaona kuwa ni kero maeneo ya watu ili nao wapate haki yao?

    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...