HAYATI SARAH .L. GELLEGE
Leo mama yetu mpendwa imetimia miaka 2 kamili tangu uitwe na MUNGU. 
Kwa kweli ni ngumu kuzoea kuishi bila wewe lakini tunamshukuru sana sana MUNGU kwani anazidi kutupigania na kututia nguvu kwani ndio tegemeo letu. Pengo uliloliacha kamwe halitozibika kwani tunakumbuka ucheshi wako na juhudi zako na ushauri wako katika kupambana na maisha na tuliona juhudi zako mama!!
Unakumbukwa sana na wanao Luther(Mtua), Lamson(Ipyana) na Ruth. Pia unakumbukwa sana na wajukuu zako ambao hawaachi kuuliza bibi wa Ukonga mbona haji siku hizi kwani kaenda wapi? Unakumbukwa sana pia na dada zako,kaka zako,wadogo zako,wifi zako,shemeji zako,wajukuu zako,
watoto zako,wakwee zako,ndugu,jamaa,majirani na marafiki kwakweli wanakumiss sana!!!
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!!!!. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...