Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo akilionyesha bunge moja ya michoro ya miradi mbalimbali ya umeme wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti Bungeni leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Mathias Chikawe akiangalia moja ya michoro ya mradi wa umeme wakati bajeti ya Nishati na Madini ikiwasilishwa Bungeni leo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Simba Chawene akizungumza jambo na mbunge wa Mtwara mjini mhe. Hasnain Murji.
Mbunge wa Peramiho Mhe. Jenista Muhagama akizungumza na Mhe. Ally Kessy (Mb. Mpanda Kaskazini) katika kikao cha bunge leo.
Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika akisoma hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni ya Nishati na Madini leo.
Mbunge wa Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malechela akichangia hoja katika hotuba ya bajeti ya Nishati na Madini.PICHA NA ZAWADI MSALLA-MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...