Ankal akiwa na Dkt Licky Abdallah na mtangazaji Chacha Maginga wa TVT (siku hizi TBC1) wakati wa uchambuzi wa mechi za Kombe la Ulaya (UEFA Championship) kwenye stesheni hiyo mwaka 2004 zilizofanyika Ureno (Portugal).
Euro 2004, kama
ilivyojulikana, ilikuwa michuano ya 12 kwa timu za Taifa za soka za wanaume za
Ulaya zilishindana, na kwa mara ya kwanza ilifanyika Ureno toka Juni 12 hadi
Julai 4 katika miji minane tofauti ya Aveiro, Braga, Coimbra, Guimarães, Faro/Loulé, Leiria, Lisbon na Porto.
Jumla ya timu 16 ilishiriki katika michuano hiyo iliyoshuhudia
Ujerumani, Spain na Italy wakiondolewa katika hatua za makundi, ambapo bingwa
mtetezi, Ufaransa, aliondolewa na Ugiriki katika robo fainali,na wenyeji Ureno
wakazinduka baada ya kufungwa kwenye mchezo wa ufunguzi na kufika fainali, kwa
kuwafunga Uingereza na Netherlands.
Mwaka huo kwa mara ya kwanza
ikashuhudiwa fainali ikizikutanisha timu zilizofungua dimba (wenyeji Ureno na
Ugiriki), ambapo Uguriki walishinda na kushangaza wengi kwani waliwahi kufuzu
mara mbili tu katika michuano mikubwa – Euro 1980 na kombe la dunia mwaka 1994.
Na ushindi wao katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Ureno ulikuwa wa kwanza katika
michezo yote ya fainali waliyowahi kucheza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...