Na: Eliphace Marwa – Maelezo
CHAMA
cha wauguzi Tanzania kinatarajia kufanya maadhimisho ya siku ya
waaguzi duniani mei 12 ambapo kitaifa yatafanyika mkoani Rukwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Rais wa chama hicho
bwana Paulo Magesa alisema maadhimisho hayo yatafanyika tarehe 12 mei
ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Kuziba pengo kufikia Malengo
ya Milenia namba 6,5,4”.
Bwana
Magesa alisema malengo hayo ya millennia yanalenga kuzuia vifo vya
mama wajawazito wakati wa kujifungua , kuzuia vifo vya watoto wenye umri
chini ya miaka mitano na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto.
“Pamoja
na changamoto nyingi tunazokutana nazo wauguzi bado tunajitahidi kwa
kadri ya uwezo wetu kuhakikisha huduma bora zinawafikia walengwa na hii
imeleta mafanikio makubwa kwani vifo vya mama wajawazito pamoja na
watoto vimepungua sana”, alisema bwana Magesa.
Wizara
ya afya na ustawi wa jamii kwa ajili ya kuzuia na kupunguza vifo vya
mama wajawazito na watoto nchini chini ya mpango huu umelenga
kuhamasisha akina mama kutumia njia salama za uzazi wa mpango na
kuhakikisha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za mama na
mtoto.
Aidha,
kwenye maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho kuanzia tarehe 10 hadi 12
mei yakionesha shughuli mbalimbali za kitaaluma wanazozifanya wauguzi
ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kiafya kama huduma ya mama
na mtoto, huduma za kupima VVU na ushauri nasaha na huduma nyingine
nyingi.
Chama
cha wauguzi Tanzania (TANNA) ni chama kinachowawakilisha wauguzi na
wakunga wote Tanzania bara na Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein
Mwinyi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...