Salaam,
Rejea dhumuni la barua hii kwako.
Kwanza niwape pole kwa tukio la ugaidi lililotokea katika kanisa katoliki Olasiti, Arusha. Nimeudhunishwa sana na tukio hili.
Asuhubi hii, baada ya kuangalia video zilizowekwa kwenye mtandao wa http://issamichuzi. blogspot.com/ nimeona ni vyema nami kuwashirikisha MTAZAMO wangu katika kuhakikisha wahusika wanapatikana.
Kwanza kabisa, mtazamo wangu nimeanza kuujenga kwa njia ya ELIMINATION.
Mhusika HUENDA hakuwa na dhumuni la KIDINI. Maana kunamakanisa mengi yalikuwa na ibada siku ile, na bila shaka kwa shughuli ile kulikuwa na uwezekano wa kuwa na mapolisi/wanausalama katika kanisa la Olasiti kwa kuwa ilikuwa ni shughuli kubwa iliyomjumuisha balozi wa Papa nchini. Kwa hiyo, kwa mtazamo wakulipua wakatoliki, mhusika ange-TARGET parokia nyingine. Hivyo nashawishika "the motive behind" HAIKUWA UDINI.
Kwa kuwa mhusika, alitupa bomu kwa mkono na kwakuwa bomu lilirushwa nje ya kanisa (walipokusanyika waumini), wakati viongozi wa kanisa wakiwa ndani ya jengo la kanisa (I just assume). Nashawishika kwamba, "the motive behind" HAIKUWA KUWADHURU VIONGOZI WA KANISA. Nikiwa namaanisha Maparoko na Balozi wa Papa nchini Tanzania.
Kwa ku-ELIMINATE hayo mambo mawili, nashawishika kuwa "the motive behind" ILIKUWA ni KUVURUGA na KULETA MAJONZI KATIKA SHUGHULI NZIMA YA KUSHEREKEA UFUNGUZI WA KANISA LILILOJENGWA KWA MIAKA 7.
KWA HALI YA NCHINI MWETU NIIJUAVYO, moja ya jambo linaloweza pelekea dhumuni la kuharibu shughuli nzima pamoja na kuua na kujeruhi waumini wengi YAWEZE KUWA ni MIGOGORO ya ARDHI (iliyotumika kujengea kanisa hilo) au MGOGORO WOWOTE uliotokea katika kipindi kizima cha UJENZI WA KANISA.
HIVYO BASI, nikiwa kama raiamwema, MKATOLIKI napenzekeza: UCHUNGUZI WA KINA UFANYIKE KATIKA HISTORIA YA UJENZI WA KANISA HILO, YAANI KWA KIPINDI CHOTE CHA MIAKA 7 IKIWEZEKANA MIAKA 10 KABISA.UCHUNGUZI HUU UJIKITE KATIKA KUTATHIMINI MIGOGORO ILIYOTOKEA na WAHUSIKA KATIKA MIGOGORO HIYO WAHOJIWE NA KUCHUNGUZWA KWA KINA.
Naamini, kwa utaratibu huo nilioupendekeza, yaweza saidia kupata muhusika wa MLIPUKO KATIKA KANISA KATOLIKI OLASITI.
Nawatakia kheri katika kuhakikisha MHUSIKA anapatikana na kufikishwa katika vyombo husika.
Una hoja lakini mazingira tuliyomo sasa hivi hakuna atakayekuelewa.Ingekuwa tukio la kwanza sawa,lakini 1,2,3.....Ngoma hii ni UDINI mwanangu,acha propapaganda hizo,acha waTanzania tuungane tuudhibiti udini na ukabila,nk.Mungu ibariki TANZANIA
ReplyDeletewewe macho yako yamefunguka nakuunga mkono asilimia mia. natumai wahusika wataangalia motive kwa njia yenye fikra zaidi kama hizi badala ya kutumia siasa na conclusion zisizokuwa na uthibitisho halisi. ahsante mdau kwa kuandika hii na pia kwa michuzi kutuwekea.
ReplyDeleteNingependa kumuunga mkono mpelelezi aliyeandika mawazo yake hapo juu. Al awal, napenda kutoa mkono wa rambirambi kwa wote waliotiwa majozi kwa tukio hili.Nimejaribu kufuatia tukio hili na kwa ufupi naona ni kitendo "unreasonable" Naona pia kiini cha sababu bila shaka si kuwadhuru wakatoliki waliokuwa kanisani, nionavyo mimi kama hiyo ingekuwa nia, huyo jamaa angeingia ndani ya kanisa na angefanikiwa zaidi kufanya madhara, basi kama mtaalam alivyosema hapo juu, kuna sababu nyingine. Nionavyo mimi hiki ni kitendo cha mtu, au watu waliodhulumiwa. Ningeomba wachunguzi wapekue kila kona ya chanzo cha ujenzi huo,na matatizo yote baina ya kanisa na raia na majirani wa kanisa hilo.Tanzania ni nchi "peaceful" and will remain so, its in our blood.
ReplyDeleteWewe mwenyewe haujui nini kilichopo ndani wala hauna ushaidi. Wala upepelezi haujakamilika, utasemaje hiyo ndiyo sababu au siyo?!! Katika upelelezi wowote kawaida wapelelezi wanaanza na hisia fulani(kisio) ndiyo unajenga ushaidi ulio kamili. Mimi nangojea uchunguzi ufanyike ndiyo nijue nini kweli kinaendelea.
ReplyDeleteKama una-asume kuwa kulikuwa na mgogoro wa ardhi wa eneo husika,kwanini aliyetupa bomu asitumie muda woote alokuwa nao kabla ya uzinduzi tena kwa nafasi bila woga na bla kuonekana na watu mpaka asubiri siku ya uzinduzi na siku ya kusanyiko la watu wengi?Si angeharibu kanisa peke yake tofauiti na sasa ambapo ameleta madhara makubwa ya wasiohusika?
ReplyDeleteNafikiri wewe ni moja ya hao watu ambao hawataki kukubali kuwa "Tanzania kuna tatizo la vurugu za kidini" Ukubali au la lakini usitake kupoteza mawazo ya wakristo wengi na Waislam wengi wapendaamani- kuwa hilo lilikuwa ni tendo zidi ya Kanisa Katoliki na waumini wake.
ReplyDeleteMpaka kufikia kujengwa kwa kanisa hapo ina maana documents zote za ujenzi wa kanisa zilikuwa OK;Kwa habari yako basi police/mahakamani hakuna hata kesi moja kuhusu kiwanja mahali kanisa lilipojengwa!Hivyo acha kuanza tafuta sababu za kuficha nia ya serikali kutokubali kuwa hilo ni mfululiuzo wa vurugu za kidini just the same as the killing of Fr.Everest Mushi in Zanzibar;au video kama hii kwenye internet http://www.youtube.com/watch?v=tjBqVRH9SzQ
So please don'nt mistake religious terrorism for civil criminal cases; and that is common for non-professionalism in Tanzanian officials. Kwa nini asiende kutupa hilo bomu sokoni au kwa wale waliomchukulia arthi? No!! akachagua kanisani walipokusanyika waumini na viongozi wao.
Mdau wewe uliyeweka hoja unajihita mkatoliki,kweli kuna dini inayosema kuua wengine hata kama umedhurumiwa ardhi?kwa mujibu wa utabiri wako kuwa kuna tatizo la ardhi basi angefuata vyombo husika na sio kurusha bomu....kulikuwa na issue ya kuchinja,paroo kuuliwa zanzibar,Ijumaa kuwa siku ya fujo dar,na hili la bomu,makanisa kuungua mbagala,dogo kukojolea quran,hapo kuna tatizo tena tatzio hiloo ni udini tunapaswa kuungana kukemia huo ujinga wa wachache,Nchi yetu haina dini ila watu wake wana Imani zao kwa kuheshimiana na kuthaminiana tutaishi kwa amani na upendo na sio hizi nyufa zilizopi.Tuungane kupinga udini kwa hali na mali sio kitu kizuri.Naomba kuwakilisha.
ReplyDeleteHakuna cha mgogoro wala nini ni udini mtupu sasa hao waarabu waliokamatwa ni vipi? Acheni kuwaona watanzania hajui kitu. Mungu atajibu. Kama ni mgogoro hao walioyopoteza maisha na majeruhi inawahusu nini.
ReplyDeletekwa kweli said nimekuunga mkono kwa mesege yako. kwann? hawakufanya kabla ya uzinduzi wa kanisa. 100% bila kuogopa ni hawa wasiotupenda ila mungu anatupenda sisi mungu ibariki Tz, Mungu tubariki wanao/ wakristo. Amen
ReplyDeleteNadhani huu sio wakati wa kulumbana wananchi, sote tuungane kuwatia nguvu wa hanga wa janga hilina kulaani kwa aliyefanya hivi akiwa na dhamira yoyote ile, iwe ni udini au mgogoro wa ardhi,na sisi tuwaachie wataalam wa mamboya upelelezi wafanyekazi yao na watupe taarifa kamili na waifanyie kazi, iwapo mdau yeyote ana ushahidi wowotw basi ajitokeze kwenye vyombo vya sheria akasaidie huenda ikawa mwanzo wa kujibu kitendawilihiki kinacho waumiza vichwa wanausalama na kutia hofu raia wema wa nchi hii walio zoea amanina utulivu.
ReplyDeleteshukrani sana, yangu ni hayo tu....Mungu ibariki Tanzania.
Sawa labda ni kweli kunamgogoro wa ardhi, Je alikuwa na mgogoro na waumini? Au mgogoro huo unatatulika kwa mabomu tu? Je waliopoteza maisha na waliojeruhiwa wanahusika na mgogoro huo? kama hivyo vyote sivyo maswali ni kwanini alifanya hivyo, dhamira ya kufanya hivyo, kusudi la kufanya hivyo, matokeo ya kufanya hivyo na kwanini iwe wakiti huo.
ReplyDeletewee uliyeweka hayo maoni, nia yako ni nyingine, na niya yako ni kusema kwamba the act was not religious motivated, ingelikuwa vema ungelinyamaza, kwa sababu hiyo math uliyoifanya hapo haimeki sense.
ReplyDeleteif you try to bring more of the explanations that you just gave, you will end up infuriating more people here.
The person that wrote the article, sounds really stupid, and probably thinks the audience are stupid as he is. I also wonder his level of education, cause he wouldn't put out such a stupid reasoning. kwanza unujua kazi ya upelelezi wewe, what elimination are u using here? are u trying to use what the bostonians police and FBI used to drill down the suspect? Vita vya kidini vimekuwa vikiendelea Tanzania kwa muda mrefu sasa, its a high time them to be address, its sad it had to take the loss of innocent life for viongozi to open up their eyes.
ReplyDeleteMuhusika mkuu anatoka Saudia, full stop, now connect the dots, id.., what are u trying to cover up here?
ReplyDeleteAddress the issue as it is, and don't beat around the bush, go were the smoke comes from.
Kwa nini unajichosha ku assume na ku speculate wakati uchunguzi unafanywa na jibu litajulikana hivi karibuni? Sasa assumptions na speculations zako zitasaidia nini kwenye kushughulikia hili tatizo? Si wewe tu, kila mtu ana mtazamo wake kwa hili jambo na kama Rais alivyosema, ni bora tusubiri tu majibu ya uchunguzi.
ReplyDeleteNimeusoma ujumbe wako na pale unapojiita wewe ni mkatoliki halafu ukaweka jina anonymous unaleta walakini kidogo. huyo mtu yawezakana kabisa alitaka kudhuru hata mapadre na maaskofu ila labda alikosa muda wa kufika pale alipotaka na pia yawezekana kabisa kuwa alikuwa na lengo la kuua wengi labda Mungu pekee anafahamu kwanini wengi hawakudhurika. Kama Rais na Cardinal Pengo walivyosema badala ya kuanza kuhisi na kujifanya makachero kama wewe mwandishi wa hii habari bora tuachie vyombo vya usalama. Nadhani kwa ujuzi wako wa Ukachero unaweza pia kutueleza kuwa yule aliyemkosa kumuua padre kule zanzibar pia alikua hana nia ya kumuua ila labda kilikuwa kiwanja na alikua anamtisha tu yule Padre. Na pia wajua nini kilitokea badala ya kumkosa yule padre mwingine hakubahatika na hiyo habari yako ya kiwanja unayotaka sisi tuiamini, utailinda vipi kukitokea tukio jingine kama lile la zanzibar ambapo watu wengi walikIfa. Ndugu sijui kama huwa unafuata vyombo vya habari jiulize pale Boston siku ile walikua watu wangapi na kwanini idadi ndogo ya watu walikufa? Je wale jamaa walikua hawataki kuua wengi? NDUGU WAKRISTU KAMA PAROKO ALIVYOSEMA FUATENI MAFUNDISHO YA DINI YENU YANAYOSEMA UKIPIGWA SHAVU LA KUSHOTO MGEUZIE NA LA KULIA MARA ZOTE VISASI HULETA MAAFA MAKUBWA. TUMSIFU YESU KRISTU
ReplyDeletekjwa hiyo ulikuwa unataka atupe mabomu siku hiyo katika makanisa yote, ndio uthibitishe kwamba ni vurugu zenye mtazamo wa kidini? basi subiri na utayaona! acha kuongea utumbo wewe
ReplyDeleteNdugu inawezekana, lakini ikawa si sababu. Kwa nini makanisa? kwanini padre? kwa nini watu waliokaa nje ya jengo na si walio ndani, kwa nini? Kuna mambo mengi ndani yake
ReplyDeleteWaarabu waliokamatwa suala lao ni kuwa walionekana wakisafiri kwenda Nairobi kutokea Arusha siku moja baada ya tukio,,,sasa hapo huwezi kusema wao ndio Wahusika.
ReplyDeleteIsipokuwa wamekamatwa ili kusaidia Uchunguzi kufanyika.
MSILETE DHANA YA UDINI MOJA KWA MOJA KWA KUWAONA WAARABU WAPI CHINI YA ULINZI NA KWA SABABU MHANGA ALIYEELEKEZEWA MADHARA NI KANISA...FBI WENYEWE WAMEKUJA NA WATAONA.
Muangalie upande wa pili wa Safaru kama Mtoa Makala anavyosema kuhusu Migogoro iwe ya Kiuchumi kama ardhi ama Siasa ama hata pia Masalahi ya Kanisa kwa kuwa ni WAZI TAASISI ZA DINI ZOTE MAKANISA NA MISIKITI zimekuwa kama SACCOS kwa siku hizi.
Hivyo watu wanagombea nafasi na maslahi ktk Taasisis hizi kama mipira ya kona.
Je mtakataa hapo?
MAWAZO YANGU, KILA MTU ANA HAKI YA KUTOA MAONI YAKE KWA JINSI ANAVYOFIKIRIA, LAKINI WATOA HOJA AU WACHANGIA MAWAZO WOTE HAPO JUU MBONA HAMNA HATA ALIYEGUSIA MANENO ALIYEONGEA KADINALI PENGO MAJUZI NA JUZI KUHUSU TUKIO ZIMA KWA MTAZAMO WAKE YEYE NA ANACHOKIJUA YEYE KUHUSU SHAMBULIO HILO, NAAMBATANISHA LINK YA ALICHOKISEMA. ALIYOYASEMA JUZI NI HAYA HAPA:- SEHEMU YA KWANZA.
ReplyDeletehttp://williammalecela.blogspot.co.uk/2013/05/kauli-ya-kadinali-pengo-yazua-maswali.html
SEHEMU YA PILI:-
http://williammalecela.blogspot.co.uk/2013/05/kadinali-pengo-afunguka-like-never.html
Analazimisha watu wakubali kuwa ni mkojo wakati wanaona ni mavi!
ReplyDeleteMwacheni jamani nadhani huko aliko ametubu kwa nini kaandika maoni hayo.Pengine nia yake haikuwa mbaya.
Tuombe Mungu sana atuongoze tuache maovu kwa kutumia dini.Watanzania tuishi kama zamani tuache kuiga mambo yanayotokea sehemu zingine .
JAMANI ACHENI MAAFA SASA NI YA WAKRISTO TU HATA UNGESEMAJE NI NGUMU IKOWAZI KABISA ILA MUNGU MUWEZA WA YOTE ATATENDA KWA MAPENZI YAKE!KISASI MWIKO KWA MIKONO YA WAKRISTU.MAANA SALA NA MAOMBI YETU NDIYO MUAFAKA WA HAYA YOTE.MUNGU KATUUMBA WOTE KWA SURA NA MFANO WAKE CHA AJABU WENGINE WANAONA WENZAO SIO ILA WAO NDIYO.
ReplyDeletewewe uliyeandika maneno aliyosema Kardinal Pengo nadhani ufikiri wako ni mdogo sana. Wewe unadhani Pengo hajasoma kama wewe aseme kuwa ulikua udini wakati akijua fika kuwa yeye ni Kiongozi wa Katoliki Tanzania hiyo itakua ni kujenga ama kubomoa? Ujue Wakristu wanatofautiana na dini zingine na ni mwiko kutumia mahali pa sala kuleta vurugu. hata kama wewe ungempiga risasi padre kanisani usitegemee kabisa kama askofu atatoa tamko la kukuua wewe, zaidi atasema wakusamehe hulijui ulitendalo. maana ni tofauti na Imani yao. Unakumbuka Pope John Paul II alimsamehe mtu aliyetaka kumuua na akamtembelea jela? Unadhani sheikh Ponda si angeanzisha kikosi chake kama mtu kuchoma korani anasababisha kanisa kuhomwa moto je tukio kama hili litakua na matokeo gani? Ni masheikh peke yao wanatoa FATWA siyo viongozi wa wawakristu.
ReplyDelete