Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakiangali Picha Mfano wa majengo ya Drum Tower Hospital ,walipokuwa wakitembelea sehemu mbali mbali za ofisi ya Hospitali hiyo,katika ziara ya Kiserikali nchini China,kwa mualiko wa Serikali ya jamhuri ya Watu wa Nchi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiapata maelezo kutoka kwa Prof Zhou Chang,wakati alipotembelea sehemu za Uchunguzi wa Afya ya binadamu kwa kutumia kompyuta maalum katika Drum Tower Hospital,Mjini Nanjing katika jimbo la jiangsu kwa ziara ya kiserikali. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake,pia na Uongozi wa Drum Tower Hospital,baada ya kumaliza kutembelea Ofisi pamoja na Sehemu mbali mbali za kutoa huduma ya Afya,akiwa katika ziara ya mualiko wa Kiserikali nchini China.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2013

    Wachina wako makini sana kuitumia vyema fursa wazipatazo kwa kutangaza wanavyoviunda kwa malengo ya kibiashara mara watembelewapo na viongozi wetu wawe wa vyama au serikali.Na sisi nao tupo makini kweli kutumia fursa kama hizo tutembelewapo kwa kulia njaa na kuomba misaada.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...